Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 26, 2025 jijini Dar es Salaam, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amesema kumekuwapo na msisitizo mkubwa wa kulinda amani nchini huku haki ikisahaulika.
Amesema ni muhimu kutambua kuwa amani ya kweli haiwezi kuwepo bila haki na kwamba msisitizo wao kama Tanganyika Law Society (TLS) ni kuuangalia Uchaguzi katika msingi wa haki, amani na utulivu