Mwabukusi: Kuna Wakili alipigwa Mahakamani kama wanaua nyoka, wengine wakasema ‘eti huyo ni CHADEMA”

Mwabukusi: Kuna Wakili alipigwa Mahakamani kama wanaua nyoka, wengine wakasema ‘eti huyo ni CHADEMA”

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Rais wa TLS, Wakili Boniface Mwabukusi amesema hayo tarehe 30 Aprili 2026 wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu uliofanyika AICC jijini Arusha.

Anasema tukio la ajabu kabisa, wakili mmoja alikuwa akipigwa mahakamani kama watu wanaua nyoka. Niliona wakipiga wakili Mahinyila. Na wengine ukiwauliza wanakuambia, 'yule ni CHADEMA.' Kuwa CHADEMA hakuruhusu wakili kupigwa.

Kwa sababu wakili huruhusiwi kuwa kiongozi wa chama cha siasa na ukawa kwenye Governing Council, lakini ukiwa wakili wa kawaida uko CCM sawa, uko CHADEMA sawa, vaa sare za chama chako utakavyo ili mradi usichanganye profession na chama chako.

Tuliona matukio kama haya, lakini ukweli nashukuru kwamba baada ya tukio kama hili tumechukua hatua kubwa sana za kulifanyia kazi. Lakini baadhi ya mambo ambayo yanatuumiza bado sisi kama mawakili na tunatakiwa tuyajadili na kuyatazama bila hofu ni wanachama wenzetu. Unajua mti mbichi ukitendewa visivyo, inakuwaje kwa mti mkavu?
 
Kama wakili (mjuvi wa sheria) anapigwa, tena mbele ya muhimuli (unao tafasiri sharia)..... nani yupo salama??
 
Back
Top Bottom