Akizungumza na Jambo TV leo Januari 09.2025, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi amesema ni vyema Mahakama ikakubali kwenda sambamba na ukuaji wa teknolojia Duniani ulivyo kwa sasa ambapo kufanya hivyo haiwezi kuwa tatizo linaloweza kuathiri mwenendo wa kesi, isipokuwa itatengeneza uwanja mpana wa wananchi kufuatilia yanayoendelea Mahakamani. Ameishauri Mahakama kutoa vibali kwa vyombo vya habari kurusha mubashara yanayoendelea katika kesi zinazoendeshwa mahakamani
"Chombo cha habari kinachotaka kipewe kibali, kipewe utaratibu kirushe, Mahakama isipende kuendesha mambo gizani, hii Mahakama imeanza mwaka 1920 ambapo hakukuwa na hivyo vitu lakini sasa hivi tupo kwenye digital world" -Wakili Mwabukusi