Mwabukusi: Msajili wa Vyama, sajilini vyama vya Gen Z, msipofanya hivyo wataunda Vikundi vya Waasi!

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, ameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuongeza usajili wa vyama vipya ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya kushiriki katika siasa.

Mwabukusi amesema vijana wanapaswa kupewa fursa ya kuwa na vyama vinavyoendana na mitazamo na lugha yao, akisema hatua hiyo inaweza kuwapa nafasi ya kujihusisha na siasa kupitia njia rasmi. “Mheshimiwa Msajili, ambalo ninaloliomba kwa dhati, sajilini vyama,” amesema Mwabukusi.

Screenshot_20261007-123035~2.png
 
na wazee nao watataka chama chao.kisha kina mama nao watake ....wazo batili hilo hao genz kwan hawako kwenye vyama vilivyopo saiv ?au mnataka uraisi wa kuwakamata kwa pamoja
 
Hujaelewa wapi?

Anamaanisha vyama vya sasa haviwakilishi mahitaji ya kizazi cha sasa... watoe nafasi kusajili vyama vya vijana vipate fursa kuwakilisha hoja na kutunga sera zinazoendana na dunia ya sasa.
Haujaelewa nini hapo?
 
Sasa hoja sio kusajili hoja ni kusema vyama ambavyo vimesajiliwa vinatakiwa kutoa nafasi nyeti Kwa Gen Z ili na wao watoe ya Rohini. Kwasababu ukisema usajili vyama vya GenZ je Kila generation ikataka chama chake itakuwaje?
 
Kwa mantiki yake, vyama vya sasa havizingatii, haviwapi nafasi na havifanyii kazi matakwa ya wananchi, hasa Gen Z. Kwa iyo kwa upande wake yuko sawa pia
 
Machawa hao hawana matakwa, ni vilaza. Hawana hoja wala nia na taifa. Ila kuna vijana genuine wapo na mawazo, wenye fikra chanya na nia ya kuongoza taifa ila nafaasi hawapati. Chama tawala kina warithi ambao ni watoto wa vigogo na inaua nafasi ya watanzania wengine kushiriki katika kujenga taifa
Una uhakika? Tatizo ni kwamba vyama vinatayarisha machawa na siyo wanasiasa
 
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, ameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuongeza usajili wa vyama vipya ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya kushiriki katika siasa.

Mwabukusi amesema vijana wanapaswa kupewa fursa ya kuwa na vyama vinavyoendana na mitazamo na lugha yao, akisema hatua hiyo inaweza kuwapa nafasi ya kujihusisha na siasa kupitia njia rasmi. “Mheshimiwa Msajili, ambalo ninaloliomba kwa dhati, sajilini vyama,” amesema Mwabukusi.

Kwani huyu ndiye Rais wa wanasheria wa huko Tanzania?
 
CCM wanaweza kukianzisha kama tawi lao halafu kikawa cha kichawa kama act, uki control uongozi umecontrol chama.
Besides hoja ya mwabukusi haina mashiko kwasababu vijana wana nafasi kwenye vyama tayari, mfano bavicha ndani ya chadema, au uvccm.
 
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, ameiomba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuongeza usajili wa vyama vipya ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya kushiriki katika siasa.

Mwabukusi amesema vijana wanapaswa kupewa fursa ya kuwa na vyama vinavyoendana na mitazamo na lugha yao, akisema hatua hiyo inaweza kuwapa nafasi ya kujihusisha na siasa kupitia njia rasmi. “Mheshimiwa Msajili, ambalo ninaloliomba kwa dhati, sajilini vyama,” amesema Mwabukusi.

Sahihi kabisa mkuu.
 
Mbona CCM itatengeneza vyama lukuki mpaka msajili ataishiwa madaftari.
 
Hii mikutano imeshakuwa michongo, imekuwa mingi sana na hatuoni matokeo yoyote
 
nani kawazuia vijana kuunda chama?
 
Back
Top Bottom