Mwabukusi: Ni huzuni sana, Taifa letu limepoteza tunu zote na tunawekeza katika Chuki, Ulaghai, vitisho na kutowajibika

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
MAANDIKO YANASEMA...TUTAWAGUNDUA KWA VINYWA NA MATENDO YAO.

Natamani iwe kama Usajili ili tusajili Wabunge hawa wawe ndani ya Bunge letu na taasisi zenye dhamana ya kulinda Utu na Uhai wetu. Taifa letu lilisifika kama nchi ya Mstari wa Mbele katika ukombozi wa Afrika tukihubiri haki na uhuru wa Kujitawala.

Ni huzuni sana kwamba kwasasa Taifa letu limepoteza tunu zote na tunawekeza katika Chuki,Ulaghai,vitisho na kutowajibika.

Hapa Bunge la Ulaya limechukua jukumu la vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ni aibu lakini ni bora na hakuna ubaya Baba wa jirani anapoingilia kunusuru familia iliyotelekezwa na Baba asiye jali.

Rafiki wa kweli ni yule akufaaye wakati wa dhiki.Hawa ni Marafiki haswa wa demokrasia na Utawala bora.

Tumechelewa sana ila muda bado upo Tujisahihishe kwa kufanya linalohitajika.

UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI ndiyo njia ya kweli na Sahihi ya kuliponya Taifa.

BAK Mwabukusi.
ADVOCATE.
 
Kamwe kenge sii msikivu haya pale ubongo ukiachana na fuvu lake hivyo ndivyo watawala wetu walivvyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…