PostGE2025 Mwabukusi: Ni rahisi kuchimba Tanzanite Kinondoni badala ya Mererani kuliko kumuona Tundu Lissu gerezani

PostGE2025 Mwabukusi: Ni rahisi kuchimba Tanzanite Kinondoni badala ya Mererani kuliko kumuona Tundu Lissu gerezani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 11, 2026, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ameeleza kuwa rekodi za mahakama tangu Kisutu zinaonesha wazi kuwa upande wa mashtaka ndio umekuwa ukichelewesha kesi ya Tundu Lissu. Amebainisha kuwa kukaa mahabusu kwa muda mrefu kunamfanya mshtakiwa kukosa uhuru wa kupata matibabu, rasilimali, pamoja na mawasiliano ya kutosha na mawakili wake, jambo aliloliita kuwa "si ishara nzuri" kwa ustawi wa taifa.

"Nilitoa mfano mimi mwenyewe kama Rais nimekwahi kwenda kule, huwezi ukamuona kabisa Tundu Lissu. Ni vigumu sana kumuona Tundu Lissu gerezani. Nilimwambia mtu mmoja, ni rahisi kuchimba tanzanite Kinondoni badala ya Mererani kuliko kumuona Tundu Lissu gerezani"
​
Aidha, Wakili Mwabukusi ametoa wito kwa Mahakama ya Rufaa kusikiliza shauri lililoko mbele yake kwa uharaka ili kuondoa mashinikizo na kuhakikisha tafsiri ya haki inaonekana kwa vitendo, akisistiza haina nia ya kuingilia uhuru wa mahakama, bali inaikumbusha kutumia miongozo na mifumo yake ya kidijitali (digital platforms) kuhakikisha haki inatendeka kwa wakati

 
Sijui hii nchi imemkosea nn Mungu kutupa rais wa nchi wa kiwango duni hv!.
Kwa 'akili' yake anaamini akiweka watu ndani, kuteka na kuua ndio wananchi watalazimika kumpenda!
 
Back
Top Bottom