Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Boniface Mwabukusi, amevitaka vyombo vya dola na taasisi za usimamizi wa uchaguzi kutoa majibu ya haraka kuhusu kile alichokiita "Mauaji ya Halaiki" na upotezwaji wa miili ya raia uliotokea Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa taifa haliwezi kupona bila ukweli na uwajibikaji.
Mwabukusi amehoji hatima ya waliopotea akisema, "Tunahitaji ukweli uliokamilika; waliotekwa wako wapi na nani aliwateka?" huku akizishutumu Tume ya Uchaguzi, Jeshi la Polisi, na Ofisi ya Msajili wa Vyama kwa kuchochea chuki na vurugu za kidemokrasia zilizopelekea ndugu wa wahanga "kuzika viatu na nguo" badala ya miili ya wapendwa wao.
Aidha, kiongozi huyo amelaani uharibifu wa mali na miradi ya kiuchumi ya vijana uliofanywa na vyombo vya dola kinyume cha sheria, akihitimisha kuwa misingi ya uhuru wa maoni na haki za kumiliki rasilimali imekandamizwa, na kwamba "Haki, Ukweli na Uwajibikaji ndivyo vitaliponya Taifa."