Mwabukusi: Viongozi wa Dini kemeeni wananchi wanapoonewa, hampendi kukemea unyanyasaji ila ni wepesi kuzunguka na amani, amani...

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Viongozi wetu wa dini, kemeeni wananchi wanapoonewa na serikali inapofanya vibaya. Hususan huu kamata-kamata unaoendelea sio wa kisheria. Ni wa kinyanyasaji na ni mbaya sana kwenye taifa.

Kwa sababu mnapokemea unyanyasaji, hata pale mnapokuja kuleta wito wa amani watu bata waelewa. Ninyi wenzetu hampendi sana kukemea unyanyasaji. Lakini ni wepesi mno kuzunguka na amani, amani, amani. Amani haiwezi kuja sehemu ambapo haki inafuabazwa. Kwa sababu amani ni matunda ya haki.

Ditadini viongozi wetu wa dini kuzungumza haki na upatanisho. Acheni mambo ya amani na utulivu; yale yatakuja otomatiki. Tuzungumzie haki na upatanisho.

Tuwe sauti ya haki viongozi wa dini, kukemea wazi ukiukwaji wa haki za binadamu bila upendeleo. Kwa sababu tumeona watu wanajiita majina ya kidini wakisema wazi wana vikosi hatari kuliko ina maana kuliko hata vya majeshi wetu. Wanaunda vikosi na kuvunja wakati katiba inasema mwenye uwezo wa kuunda jeshi na kuvunja ni amiri jeshi mkuu, ni rais wa nchi.

Huyu anayeunda jeshi lingine ni nani? Anayesema mimi nimeunda jeshi hili, nimevunja leo, sijui nimefanya nini, lakini wana majina ya kidini hatuwaoni viongozi wa kiroho wakikemea, wako kimya. Lakini viongozi hawa hawa utawakuta kesho 'amani na utulivu' labda kwa sababu kijana fulani kakosao jambo fulani kwa namna ambayo haijapendeza serikali, wanaanza kujaribu kufanya. Kwa hiyo viongozi wa dini wasimame kwenye nafasi yao kuwa sauti ya haki. Lakini kusimamia maadili..."

Pia soma: PostGE2025 - Mjadala wa wazi Kati ya Viongozi wa Dini na Wananchi kuhusu Amani na yaliyotokea Oktoba 29, 2025
 
Dini ni utapeli

Hicho wanacho kifanya viongozi wa dini ndio reason ya kuundwa kwake,

So they're on the right track Kwa Mujibu wa kuanzishwa kwake
 
Sahihi ✔️
 
Back
Top Bottom