- Source #1
- View Source #1
Naombeni kujua hii una ukweli wowote?
- Tunachokijua
- Madai
Agosti 25, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii imesambazwa grafiki yenye utambulisho wa vyombo vya habari vya Mwananchi na Mwanahalisi ikiwa na taarifa kuwa
"Mwabukusi: Watanzania wana wajibu wa kidemokrasia kushiriki uchaguzi"
Grafiki hiyo imeambatana na inayoonekana kuwa ni 'screenshot' ya ujumbe uliochapishwa na Rais wa chama cha mawakili Tanganyika (TLS), Bonifase Mwabukusi akieleza mambo mbalimbali ukkwemo kusema maamuzi ya CHADEMA kutoshiriki uchaguzi hayawezj kuchukuliwa mama maamuzi ya Watanzania wote.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia ufuatiliaji kwa njia ya utafutaji wa maneno muhimu, JamiiCheck imebaini kuwa ujume unaonekana kwenye 'screenshot' haujachapishwa na Mwabukusi kupitia ukurasa wake wa X kama unavyoonekana na badala yake ni wa kughushi.
Aidha ufuatiliaji kwa njia ya mtandao umebaini kuwa grafiki hizo zenye utambulisho wa Mwananchi na Mwanahalisi hazijchapishwa na vyombo hivyo vya habari.
Aidha grafiki hiyo ina mpangilio tofauti wa uandishi ukilinganisha na ule unaotumiwa na Mwananchi katika grafiki zao halisi