Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Rais wa Tanganyika Law Society (TLS) Boniface Mwabukusi, amesema Waziri hana Mamlaka ya Kufuta Vijiji vya Ngorongoro
Ameyasema hayo leo 20/08/2024 Mkoani Dar Es Salaam alipokuwa anaongea na Waandishi wa habari. Amesema kama TLS wanaaangalia cha kufanya. "Wale wananchi wa Ngorongoro hawapaswi kupuuzwa, Warudishiwe huduma Muhimu pia Warudishiwe vituo cha kupigia Kura. Ni lazima tujue chanzo cha Tatizo Ngorongoro ni nini?". Amesema Mwabukusi
Mwabukusi amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwakamta wabakaji na kuwafikisha Mahakamani. Amesema kuwafikisha mahaksmani ni hatua ya kwanza, ametaka Polisi imfikishe Mahakamani aliyewatuma pia. Pia amewata Polisi kumuachia na kumuweka wazi mwanamke alipata madhira ili haki yake ipatikane ikiwrmo kupewa msaada wa kisheria..
Stsy tuned
=====
20 Agosti, 2024
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimepata taarifa kupitia mitandao ya kijamii kwa njia ya video iliyosambaa kwenye mitandao hiyo ikionyesha maandamano yaliyofanywa mnamo tarehe 18 mwezi Agosti, 2024 na mamia ya Wananchi wa Ngorongoro wakidai kuheshimiwa kwa haki zao. Katika maandamano yao miongoni mwa mambo mengine, Wananchi hao wamesikika wakilalamikia kuondolewa kwenye maeneo yao kinyume na utaratibu bila wao kuridhia pamoja na kuondolewa kwa huduma zote za kijamii kama vile shule, huduma za afya pamoja na maji. Kutokuwepo kwa huduma hizi muhimu kumepelekea Wananchi hao kuendelea kuishi katika mazingira magumu.
Tamko la Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Watu wa Asili la Mwaka 2007 limeeleza wazi katika ibara ya 10 kwamba watu wa asili hawataondolewa kwa nguvu kutoka kwenye ardhi au maeneo yao, uhamisho wowote wa watu wa asili hauwezi kufanyika bila idhini yao huru
Kwa mujibu wa ibara ya 24 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kila mtu anayo haki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo. Haki ya kumiliki mali ni moja ya haki ya msingi ya binadamu. Ibara 24 (2) imeeleza wazi kwamba mtu yoyote hatonyang’anywa mali yake isipokuwa kwa kuzingatia taratibu za kisheria ikiwepo ulipwaji wa fidia stahiki.
TLS inatoa rai kwa Serikali kuonyesha nia yake ya dhati kwa kurudisha huduma zote za kijamii kwa Wanachi wa Ngorongoro kwa kuwa ni haki yao. Pia, vituo vya kujiandikisha kwa ajili ya kupigia kura ambavyo Wanachi wa Ngorongoro wanalalamika kwamba havipo katika maeneo yao virudishwe ili wapate kuitumia haki yao ya kikatiba ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopangwa kufanyika mwezi Novemba mwaka 2024 pamoja na Uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2025.
Baraza la Uongozi la TLS limeona jambo hili la Ngorongoro na maeneo mengine linahitaji ufuatiliaji wa kina zaidi na kwa sababu hiyo, Baraza limeamua kuunda kamati maalum itakayofuatilia jambo hili kwa ukaribu ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na Idara, Wizara na vyombo vyote vinavohusika na suala la Ngorongoro ili kujua ukweli zaidi na kuhakikisha misingi ya sheria za nchi yetu inafuatwa.
Kamati iliyoundwa inajumuisha wajumbe wafuatao:
*Dr. Rugemeleza Nshala
*Tike Mwambipile
*Bumi Mwaisaka
*Laetitia Petro Ntagazwa na
*Paul Kisabo.
Miongoni mwa mambo mengine kamati itafanya mambo yafuatayo:
*Kufanya mashauriano na taasisi mbalimbali pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo yenye migogoro ili kujua uhalisia wa migogoro husika.
*Kufanya Mapitio ya Sera ,Sheria na Mazoea pamoja na kuzichambua kuhusiana na umiliki wa Ardhi kwa Wazawa pamoja na shughuli za uwekezaji na Uhifadhi na kubaini uzingativu wa Haki za Msingi za Raia katika maeneo husika kwa kuzingatia Katiba, Sera na Sheria za Nchi.
*Kuandaa kongamano (Symposium) la Kitaifa kuhusiana na namna bora ya kufanya maendeleo kwa kuzingatia na kulinda haki za Wazawa katika Ardhi zao za Asili pamoja na haki zao za Kijamii, Kiuchumi na Kiutamaduni katika maeneo yanayofikiwa na shughuli za uwekezaji.
*Kubaini mashauri au hatua zote ambazo zimechukuliwa na walalamikaji pamoja na walalamikiwa kisheria na kiutaratibu katika kuhakikisha uzingativu wa sheria na kubaini majina ya watu ambao kweli wameridhia kuondoka kwa hiyari kwenye maeneo yao na ambao hawakuridhia kuondoka kwa hiyari kwa sababu ya wao kuamua kubaki katika eneo lao la asili Ngorongoro.
*Kubaini na kulishauri Baraza la Uongozi la Chama Cha Mawakili wa Tanganyika juu ya hatua zakuchua ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu swala la migogoro ya Ardhi inayosababishwa na mipango ya uwekezaji au uhifadhi.
Kamati inatarajiwa kumaliza kazi tajwa ndani ya muda wa kipindi cha siku 30.
TLS inawaomba Wanachama, Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Sheria kutoa ushirikiano kwa Kamati maalum iliyoundwa ili TLS kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria iliyounda TLS (Tanganyika Law Society Act Cap. 307) iweze kutimiza wajibu wake wa kuishauri Serikali na Kulinda haki za Wananchi kwa lengo la kupata suluhisho la kudumu.
Imetolewa na Baraza la Uongozi la Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
Boniface A.K Mwabukusi
Rais

TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU WITO WA WANANCHI WA NGORONGORO NA MAENEO MENGINE KUTAKA KUHESHIMIWA KWA HAKI ZAO