Mwadui FC yamumunywa na Simba SC Kambarage, Mwadui 0-3 Simba

Mwadui FC yamumunywa na Simba SC Kambarage, Mwadui 0-3 Simba

Kikosi kinachoanza leo.

1477736781028.jpg
 
Simba atashinda tu ata na mechi ya stand ratiba imewanyonga stand make wanacheza mechi kesho pwani,jumatatu wanageuza kisha jumatano mechi.
Hujajua kuwa msimu huu wamewekewa mazingira?? But wataishia nafasi ya pili
 
Mkuu.. nipo mjini.. Hawa Mwadui ni wetu kabisa.. Hebu cheki takwimu hizi;

1. Sisi.
Idadi ya mechi tulizocheza: 11
Tumeshinda: 9
Tumefungwa: Hakuna
Sare: 2
Magoli tuliyofunga: 21
Magoli tuliyofungwa: 3 [ya halali 2]
Nafasi katika msimamo wa ligi: Kama Kawaida [Wa kwanza]

2. Wao.
Idadi ya mechi walizocheza: 11
Wameshinda: 3 tu
Wamegongwa: 4
Sare: 4
Magoli waliyofunga: 9 tu
Magoli waliyofungwa: 10.
Nafasi katika msimamo wa ligi: 11
Mpira unadunda ndugu!
 
Dk 14 Rashid Ismail anapiga shuti karibu kabisa na langu la Simba, unapita juu

Dk 9 Mwadui wanapoteza nafasi nyingine ya wazi hapa baada ya kupiga shuti kuuubwa

Dk 9, MWadui wanagongeana vizuri wanafunga hapa lakini Hamisi alikuwa ameishaotea

Dk 7, Mavugo tena anaichezea nafasi nyingine na kupiga juu akiwa na nafasi nzuri kama angetulia

Dk 6, Mavugo anawachambua mabeki wa Mwadui na kuachia mkwaju mkali, unatoka juu kidogo

Dk 4, bado hakuna kitu chochote ambacho kinaonekana ni mabadiliko kwa kuwa mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja.

Dk 1 Simba wameanza kwa kasi lakini shuti la Mavugo linatoka nje.
 
Dk 22 sasa, mpira hauvutii sana, hakuna timu inayoonyesha imepania kupata mabao ya haraka. Zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali
 
Dk 25, Mavugo a.k.a Zigo La Mavi anatoa krosi safi kabisa kwa Kichuya, lakini anaruka na kupiga kichwa juuuu
 
GOOOOOO Dk 32, Mo Ibrahim anamchambua beki wa MWadui na kufunga bao safi kabisa kwa Simba

Dk 31, pasi nzuri ya Kazimoto, Mo Ibrahim anashindwa kuitumia na kupiga shuti nyanya hapa

Dk 29, MWadui wanapata kona ya kwanza hapa, inachongwa vizuri na Rashid Ismail anajitwika lakini inakuwa ni goal kick
 
Ndugu yangu umelelewa na wazaz kwel kwa maneno hayo unayoyatamka? Anyway hata kama hujalelewa na wazaz ina maana hata malezi ya kawaida tu hujapata? Binadam wa kawaida hawez mwita binadam mwingine hivyo hata kama anamchukia vibaya sana.

Ushabiki wa simba na yanga usiondoe akili zetu au ustaarab.


Dk 25, Mavugo a.k.a Zigo La Mavi anatoa krosi safi kabisa kwa Kichuya, lakini anaruka na kupiga kichwa juuuu
 
Dk 35, hatari kwenye lango la Mwadui, Kazimoto anamtoka kipa na kumpa Muzamiru pasi peke yake na nyavu, anaukosa mpira unaokolewa

DK 33, Mwadui wanaingia vizuri, shuti la Madenge lakini linamgonga Angban usoni na Mwanjale anaokoa
 
Back
Top Bottom