Mwajiri alikuwa hapeleki michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii. PSSSF wanakataa kumbana kwa mujibu wa sheria

Mwajiri alikuwa hapeleki michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii. PSSSF wanakataa kumbana kwa mujibu wa sheria

mambo_safi

Senior Member
Joined
Jul 22, 2019
Posts
176
Reaction score
440
Mtumishi mmoja baada ya kuachakazi na kulipwa mafao yake (pungufu) akaanza kudai Mapunjo ya miezi karibia 12 yenye dhamani zaidi ya millioni 2 (hiki ni kiasi kikubwa).

Akafungua file la madai. Chakushangaza PSSSF inamwambia mteja wake kuwa Huyo mwajiri hataki kutoa ushirikiano wa kulipa hayo madai.

Sasa hawa PSSSF kazi yao nini kama wanashindwa kumbana na kumshinikiza mwajiri alipe mafao ambayo hakuwasilisha?

Mifuko ya jamii ndiyo iliyopewa rungu kwa mujibu wa sheria kuhakikisha mwajiri anawasirisha michango ya mwajiriwa na asipofanyahivyo anashitakiwa na kulazimika kulipa na faini juu.

Sasa PSSSF kuanza kulialia kwa mteja wake heti mwajiri hataki kutoa ushirikiano ina maana gani? Au ni mazingira ya rushwa?

Wadau mnamshaurije huyu anayedai ikiwa PSSSF wanazingua?
 
PSSSF sijui kazi yao ni nini? Hii mifuko imekaa kiwiziwizi kuiba muda na jasho la wafanyakazi!
 
PSSSF ni kwa watumishi wa umma
Kama mtu ukiacha kazi Kuna complication je alitoroka, aliaga,alitoa notice kadri Sheria zinavyosema ,alifukuzwa,alikuwa na kesi asifiche fiche scenario ili ashauriwe vizuri.Hiki alichoandika hakitoshi mtu kumpa ushauri aeleze full story
 
Mifuko ya jamii haina hiyo scenarios- hizo scenarios kwa mambo mengine kama kiunua mgongo.
 
Mifuko ya jamii haina hiyo scenarios- hizo scenarios kwa mambo mengine kama kiunua mgongo.
Mwajiri kutopeleka michango Kuna mengi Sasa Kama yeye anaficha ficha aliachaje kazi scenario ipi abaki hivyo hivyo
 
Nionavyo hoja ni hilo jibu la PSSSF kumwambia mteja wake kuwa "huyo mwajiri hataki kutoa ushirikiano wa kulipa hayo madai". Hili litakuwa ni jibu la mdomo tu kutoka kwa mfanyakazi wa PSSSF.

Hebu mhusika wa mafao awaandikie barua rasmi PSSSF kuhusu kupunjwa mafao yake na kutaja hilo jibu la mdomo alilopewa na huyo mfanyakazi tuone kama jibu rasmi atakalopewa kimaandishi litasomeka hivyo hivyo kwamba mwajiri hataki kuonyesha ushirikiano.
 
Kajaribu kwanza kuulizia kwanza kwenye kampuni uliokuwa unafanya kazi.
Possibly, Pesa yako imeingia mifuko tofauti.

Kuna Mkanganyiko wa kipumbavu umetokea baada ya mifuko kuunganishwa
 
PSSSF sijui kazi yao ni nini? Hii mifuko imekaa kiwiziwizi kuiba muda na jasho la wafanyakazi!
Yaani! Statement ya michango inaonyesha michango ya miezi yoote aliyotumikia ISIPOKUWA miezi 12 tena mfululizo mwajiri hakupeleka michango. Alipoachakazi walimlipa michango iliyopelekewa tu ikiwa na pungufu ya miezi 12 ambayo mwajiri hakupeleka. Aliambiwa baada kulipwa kilichopo kinachodaiwa utaandika barua na mfuko (PSSSF) utamtaka mwajiri awasilishe michango na atalipwa. Barua alishaandika na sasa ni mwaka wa tatu kila akienda anaambiwa mwajiri hatoi ushirikiano!!! Ushirikiano gani wakati anatakiwa kisheria kulipwa michango ya mafao?
 
Kama mtu ukiacha kazi Kuna complication je alitoroka, aliaga,alitoa notice kadri Sheria zinavyosema ,alifukuzwa,alikuwa na kesi asifiche fiche scenario ili ashauriwe vizuri.Hiki alichoandika hakitoshi mtu kumpa ushauri aeleze full story
Huko alitokaje sio hoja tena kwasababu mafao yake yaliyokuwa yamepelekwa alishalipwa isipokuwa ya miezi 12 ambayo mpaka anatoka kazini mwajiri alikuwa bado hajayapeleka kwenye huo mfuko wa hifadhi ya jamii (mapunjo)
 
Mwajiri kutopeleka michango Kuna mengi Sasa Kama yeye anaficha ficha aliachaje kazi scenario ipi abaki hivyo hivyo
Mkuuu! Alifanyakazi miaka 15. Miaka 3 na miezi 4 ya mwanzo michango ilipelekwa vizuri. Miezi 12 iliyofuata statement ikawa inaonyesha michango haiingii kwenye mfuko husika. Alipoenda kuulizia mfuko mbona sioni michango yangu, mfuko (kipindi hicho) ukamwambia utafuatilia, na baadaye michango ikaanza kuingia lakini ni michango mipya tu (sio ile ya miezi 12 iliyorukwa). Tangu hapo mpaka anatoka kazini miaka 11 baadaye ilo gepu (deni) la miezi 12 haijawahi kulipwa! Na alipokuwa kazini kila akimtaka mwajiri awasilishe michango yake alikuwa anapigwa sound. Na kama unavyojua kama huko kazini huwezi kumvuta shati bosi zaidi ya kuubana mfuko uwende kwa mwajiri ukadai kwa niaba yake
 
Munapo andika neno PSSSF Msisahu na kirefu chake maana Kuna ma younger generation Hawajui haya Mambo vizuri
 
Kajaribu kwanza kuulizia kwanza kwenye kampuni uliokuwa unafanya kazi.
Possibly, Pesa yako imeingia mifuko tofauti.

Kuna Mkanganyiko wa kipumbavu umetokea baada ya mifuko kuunganishwa
Alishatoka hapo kazini zaidi ya miaka 2 sasa na hakuna jipya zaidi ya longolongo alizokuwa akijibiwa akiwa kazini. Kama mwajiri alishindwa kupeleka michango kipindi yuko kazini ndo watamsikia wakati hayuko kazini?. Hapa ni kazi ya mfuko husika (PSSSF) kutumia mamlaka iliyopewa kwa mujibu wa sheria kumshinikiza alipe mapunjo ya mwajiriwa wake ambayo hakupeleka. Wakikaidi PSSSF ina mamlaka ya kumshitaki mwajiri.
Kama kuna mchezo ulichezwa wakazila hizo hela basi ndo maana wananyamazisha kila anayeenda kukumbushia hiyo michango!
 
Back
Top Bottom