Mwajiri alikuwa hapeleki michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii. PSSSF wanakataa kumbana kwa mujibu wa sheria

Mwajiri alikuwa hapeleki michango ya mifuko ya hifadhi ya jamii. PSSSF wanakataa kumbana kwa mujibu wa sheria

Hata akiandika barua hatajibiwa, siku hizi PSSSF ni shida
Nionavyo hoja ni hilo jibu la PSSSF kumwambia mteja wake kuwa "huyo mwajiri hataki kutoa ushirikiano wa kulipa hayo madai". Hili litakuwa ni jibu la mdomo tu kutoka kwa mfanyakazi wa PSSSF.

Hebu mhusika wa mafao awaandikie barua rasmi PSSSF kuhusu kupunjwa mafao yake na kutaja hilo jibu la mdomo alilopewa na huyo mfanyakazi tuone kama jibu rasmi atakalopewa kimaandishi litasomeka hivyo hivyo kwamba mwajiri hataki kuonyesha ushirikiano.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali, jambo hili linatuhusu wengi sana. Tunamuomba sana Waziri anayehusika atusaidie tafadhali. Tulifanya kazi kwa kujituma vizuri sana. Kwa unyenyekevu mkubwa, Waziri husika tusaidie. Mungu yupo atakubariki
 
Tafadhali, jambo hili linatuhusu wengi sana. Tunamuomba sana Waziri anayehusika atusaidie tafadhali. Tulifanya kazi kwa kujituma vizuri sana. Kwa unyenyekevu mkubwa, Waziri husika tusaidie. Mungu yupo atakubariki
Kwa mira nyingi za kiafrica (Tanzania ikiwemo) vyeo vikubwa katika ajira za makampuni na mashirika na kwenye siasa watu lazima waende kutambika kwao kwenye mizimu na waganga wa kienyeji mwisho wa siku akipata kazi kwa vile alipewa na shetani utendaji wake unakuwa wa dhuruma, kutowajibika, wizi, kutotenda haki n.k.! Inakuwaje Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF asisikie kilio cha wateja wake mpaka waje JF kujifariji?
 
Mtumishi mmoja baada ya kuachakazi na kulipwa mafao yake (pungufu) akaanza kudai Mapunjo ya miezi karibia 12 yenye dhamani zaidi ya millioni 2 (hiki ni kiasi kikubwa).

Akafungua file la madai. Chakushangaza PSSSF inamwambia mteja wake kuwa Huyo mwajiri hataki kutoa ushirikiano wa kulipa hayo madai.

Sasa hawa PSSSF kazi yao nini kama wanashindwa kumbana na kumshinikiza mwajiri alipe mafao ambayo hakuwasilisha?

Mifuko ya jamii ndiyo iliyopewa rungu kwa mujibu wa sheria kuhakikisha mwajiri anawasirisha michango ya mwajiriwa na asipofanyahivyo anashitakiwa na kulazimika kulipa na faini juu.

Sasa PSSSF kuanza kulialia kwa mteja wake heti mwajiri hataki kutoa ushirikiano ina maana gani? Au ni mazingira ya rushwa?

Wadau mnamshaurije huyu anayedai ikiwa PSSSF wanazingua?
Kifupi nikwamba Sasa hivi Rushwa inasumbua sana kwenye taasisi za serikari Na baadhi ya office zake.

Jana nimeshuhudia pale viwanja vya mnazi mmoja kwenye maonyesho ya week ya mwaka wa MAHAKAMA nchini, Bibi Mzee sana anaambiwa nawatu wa Nida arudi mahakamani kutengenezewa kiapo cha mama Yake baada yakuwa Na kiapo cha mama Yake ambacho nacho alitengenezewa Kwa tsh.6000/= wakati hapo hapo kwenye maonyesho kuna banda LA wanasheria! Mahakama zote kuanzia ya mwanzo mpaka MAHAKAMA KUU ypo kwaajiri yakutoa Huduma Kwa wananchi! Mimi naamini hii nchi saivi kunashida .

Hivyo hili LA mstaafu mi sishangai Mimi niliwahi kudai tsh.4ml. Nssf kwenye malipo nililiwa laki NNE.
Tutoeni Taarifa sehem husika badara yakulalamika Mimi huwa nawachoma maana niupunbavu.

Kesho naenda Nida kufata cheti cha Mtoto nasikia ukilipia bank unakaa 2 au 1 weeks ndo upate ila ukilipa cash ambayo kunachajuu km elf kumi hivi wanakupa hapohapo. Sasa nataka niandae Waya kesho nachoma MTU.
Km anapitia hapa aache hyo diri kesho nimikoa ya kanda ya ziwa, kesho nakinukisha wal-rah mtume.
Wametuchosha walizoea kutufanya mashamba yao wakati wao wanamishahara sisi ninguvu ztu
Waache Kazi km wanaona tunahela waje mitaani penye hela.
 
Aende mahakamani mahakama ndio itaweza kumbana mwajiri vizuri
Mimi nadhani asiende mahakamani kushitaki mwajiri. Aende mahakamani kushitaki PSSSF katika mkoa hule alipofungulia madai kwa kutowajibika kudai mapunjo yake. PSSSF ndo yenye nguvu za kisheria kushitaki mwajiri asipowasirisha michango ya mwajiriwa. Akisema anashitaki mwajiri itabidi aende mkoani katika mkoa hule alipo mwajiri hivyo itamgharimu nauli na malazi. Afungue shauri katika mkoa huo ilipo ofisi ya PSSSF kwa uzembe!
 
Back
Top Bottom