Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je, muajiri anapokataa kukuthibitisha baada ya miezi 12 kupita, si inapaswa akupe taarifa kwa maandishi kuwa ni sababu ipi imefanya asikuthibitishe kazini?Mwajiriwa ana haki ya kuthibitishwa kazin baada ya miezi 12 lakin si lazima. Mwajir anaweza kumuongezea muda wa matazamio ambao kisheria NI miez 6.
Unapaswa kusubir ipite hiyo miezi 6 ambapo ni lazima mtapewa barua za kuthibitishwa au kusitishwa mkataba.
kwa mujibu wa sheria ,muda wa majaribio au probation inapaswa isizidi kipindi cha miezi 12 na baada ya hapo itabidi mwajiri andike barua ya kukuthibitisha kazini au kukuruhusu kuondoka ,japo katika taasisi za serikali mara nyingi barua ya kuthibitishwa inaweza toka hata baada ya 1mwaka.Habari ndugu zangu,
Mimi ni mwajiriwa wa taasisi X taasisi yenye ubia na serikali, niliajiriwa mwaka jana na tangu niajiriwe nimeshamaliza muda wa maangalizi wa miezi 12 na sasa ilibidi nikafuatilie barua yangu ya kuthibitishwa kazini.
Mwajiri amekataa kuitoa kwasababu miongoni mwa wale tulioajiriwa pamoja, mmoja wapo hana maelewano nae mazuri kwakuwa alionesha nia ya kuhama taasisi hiyo mara tu atakapopata barua ya kuthibitishwa kazini, hivyo hataki kutupatia barua za kuthibitishwa kazini, anafanya kumkomoa yeye ili asiweze kuhama.
Badala yake kupitia kumkomesha yeye tunajikuta na sisi tumeingia matatizoni, tumeishaenda mara kwa mara kufuata barua hizo hatupewi tunaishia kufokewa tu.
Hasara zake ni kuwa, mwaka huu hatujapata nyongeza ya kila mwaka increment kwakuwa hatujathibitishwa kazini bado, pia tutachelewa kupanda madaraja.
Je, tufanyeje au twende ngazi ipi tuweze kusaidiwa?
NB: Hatuna kosa lolote wala hatujawai kuandikishwa maelezo yoyote ya utovu wa nidhamu ila muajiri anataka amkomoe mtu mmoja miongoni mwetu.
Asante mkuukwa mujibu wa sheria ,muda wa majaribio au probation inapaswa isizidi kipindi cha miezi 12 na baada ya hapo itabidi mwajiri andike barua ya kukuthibitisha kazini au kukuruhusu kuondoka ,japo katika taasisi za serikali mara nyingi barua ya kuthibitishwa inaweza toka hata baada ya 1mwaka.