Habari ndugu zangu,
Mimi ni mwajiriwa wa taasisi X taasisi yenye ubia na serikali, niliajiriwa mwaka jana na tangu niajiriwe nimeshamaliza muda wa maangalizi wa miezi 12 na sasa ilibidi nikafuatilie barua yangu ya kuthibitishwa kazini.
Mwajiri amekataa kuitoa kwasababu miongoni mwa wale tulioajiriwa pamoja, mmoja wapo hana maelewano nae mazuri kwakuwa alionesha nia ya kuhama taasisi hiyo mara tu atakapopata barua ya kuthibitishwa kazini, hivyo hataki kutupatia barua za kuthibitishwa kazini, anafanya kumkomoa yeye ili asiweze kuhama.
Badala yake kupitia kumkomesha yeye tunajikuta na sisi tumeingia matatizoni, tumeishaenda mara kwa mara kufuata barua hizo hatupewi tunaishia kufokewa tu.
Hasara zake ni kuwa, mwaka huu hatujapata nyongeza ya kila mwaka increment kwakuwa hatujathibitishwa kazini bado, pia tutachelewa kupanda madaraja.
Je, tufanyeje au twende ngazi ipi tuweze kusaidiwa?
NB: Hatuna kosa lolote wala hatujawai kuandikishwa maelezo yoyote ya utovu wa nidhamu ila muajiri anataka amkomoe mtu mmoja miongoni mwetu.