Mwaka 1988 Chakachaka alipiga show Makondeko Kibamba kiingilio kilikuwa 100,000

Mwaka 1988 Chakachaka alipiga show Makondeko Kibamba kiingilio kilikuwa 100,000

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Imepita miaka 35. Nimekumbuka kitu kimoja. Mwaka 1988 enzi hizo Ivon Chakachaka akiwa kwenye peak,kulikuwa na mmakonde mmoja akiitwa Dk Khalid Alex mbunge wa Mtama by then,sina uhakika na jimbo ila ni huko kusini
,alikuwa na ukumbi kule kibamba Luguruni maarufu kama Makondeko.

Ule ukumbi ukienda leo hakuna hata mabaki ya tofali hata moja ulikuwa ukumbi wa kisasa kwa miaka ile,kumbuka ulikuwa utawalawa Mzee Ruksa.

Chakachaka akiwika na nyimbo zake kama Sangoma, Umkhomboti, Thank you Mr Dj, am in love with DJ, alikuwa wa moto kwelikweli ila huyu tycoon wa enzi hizo bwana Alex akafanikiwa kumleta nchini, kiingilio kilikuwa shilingi laki moja, lakini ukumbi ulifurika haswaa japo uko nje ya mji, ni miaka 35 imepita ila laki moja.
 
Laki moja mwaka 1988?

hao waliofurika wameacha urithi gani kwa wajukuu zao mpaka sasa?

maana laki 1 ya '88 kwa sasa ni kama milioni 1. Bei ya viwanja kumi jijini Dar kwa enzi hizo
Hela ilikuwepo sana enzi za mwinyi,nzee wangu alijenga nyumba nyingi sana kipindi hicho na alikuwa kijana mdogo mwenye cheo cha chini tu serikalini, mkapa alivyoingia kukaibuka msemo kuwa kama hukujenga kipindi cha mwinyi hujengo tena, aliziba mianya yote ya upigaji,mzee alikuwa shirika la likitwa ugawaji pale ilala ofisi za NSSF,lilifia mikononi mwao, poor management.
 
Mkuu tuletee story la La Lrima Club pale Kijitonyama na Silent Inn Mwenge. Nilikuwa mdogo miaka ile ya 90's. Nakumbuka hizo kumbi zilibamba sana
LaPrima Club ilikuwepo pale Victoria ndio Alipiga Kanda bongoman mwaka, 90 kwa kiingilio cha laki wakati huo lami inaishia hapo Victoria barabara ya vumbi inaanzia hapo Victoria mpaka mwenge kuelekea huko tegeta
 
Back
Top Bottom