Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Aisee mimi ni mmojawapo... Na tulikuwa tunatoka sita tu mkoa mzima kwenda IFUNDA TECH kila mwaka... Nilijulikana ile mbaya yaani
 
Ni zaidi ya ukweli, ulikuwa huwezi kuwakalisha pamoja mwanafunzi wa Geita sekondari na wa Sengerema secondary.
 
nikweli kabisa....wale wanoenda private tuliwaita wamefail..sie wa serikali tumefaulu...lkn kwa sasa kibao kimegeuka.
 
Tulipasua vibaya saana....nakumbuka wilaya nzima tulikiwa 15 tu tulijulikana!! Moshi Tech, Bihawana, Msalato, Weruweru; Tabora Boyz / Girls....

Wakati huo elimu under Mwalimu ilikuwa na hadhi...ukiwa form one ukirudi likizo kwenye msiba kijijini basi unakaa na wazee wa heshima eee wazee wastaafu na walimu na watumishi wa Serikali kama katibu kata / tarafa; Mratibu wa Elimu etc

Sasa hivi laah form one shule ya kata anachojua ni mauno ya nandi na singeli....
 
Hiyo iko poa kama ulivyo wasilisha.

Wakongwe hua wanasema hayo yote.

Kwa sisi ambao tuko bado shule kama tunavyo ingia sekondari sana ilichaguliwa shule ya serikali kawaida ila waliopo shule binafsi ndio wanajiona wao ndio wao
 
tulitoka Burka primary school tukaenda Arusha secondary school, tulikuwa saba tu kati ya watoto mia tatu ila tulivyunja rekodi
 
Sasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge

Chuo E mbili

Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
 
Uzi umenikumbusha mbali sana, Tanga mjini miaka ya 2002 kurudi nyuma shule za secondary zilikua nne tu , Usagara Sec, Tanga school (hii ilichukua vipaji) Galanos na Mkwakwani. Yaani hapo ilikua ukichaguliwa ujue we mwanaume hasa. Shule nyingi za primary zilikua na wanafunzi wanaomaliza la 7 zaidi 100 lkn wanaochaguliwa kwenda sekondari hawazidi 20. Hivyo kujihakikishia nafasi lazima uhakikishe upo ndani ya top 10 darasani

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Kwa miaka ya hivi karibuni, hata mimi nilistaajabishwa na jinsi wizara ya elimu wanavyojitahidi kuwapangia wanafunzi shule, kutokana na ufaulu wao. Hapa naongelea matokeo ya kidato cha nne. Kulikuwa na vijana mbalimbali, wewe mikondo mbalimbali na ufaulu tofauti tofauti, kuanzia daraja la kwanza mpaka la tatu.

Nikashuhudia waliochaguliwa katika mkupuo wa kwanza, walipelekewa kidato cha tano, wengine chuoni, muda ukapita wengine wa daraja la tatu na nne wakiwa mtaani. Mara uchaguzi mkupuo wa pili ukaja, hapa waliochaguliwa kwa kuzingatia kile mtu alichofaulu, mfano mtu alifeli hesabu, uhasibu, biashara, jiografia, ila akawa na ahueni katika Kiswahili, Kiingereza na Historia. Basi akapelekwa kidato cha tano HKL.

Mwingine akapangiwa mpaka VETA, ufaulu wake ulikuwa dhaifu wa daraja la nne. Kwa kweli nilistaajabu kwa umakini huu, na nafikiri uwepo wa shule na vyuo vingi umepelekea wanafunzi kwa asilimia kubwa kupata fursa ya kujiendeleza. Ni jambo jema!

Linalonichanganya ni je, shule ziko chini wa wizara ya Elimu au Tamisemi?
 
Nakumbuka Sumbawanga mjini, mwaka 2001 kurudi nyuma, ikifika Desemba kabla ya Christmas majina ya waliopangiwa kwenda kidato cha kwanza, manispaa nzima yanabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa soko kuu. Shule yangu tulikuwa 100 darsani, tuliotoboa tulikuwa 13 tu kwenda form one boarding nje ya Sumbawanga na wengine day ndani ya Sumbawanga mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…