MrFroasty
JF-Expert Member
- Jun 23, 2009
- 1,195
- 595
Unajua hata waingereza walikuwa wakifikiria hivyo hivyo kama Nyerere akiwa kiongozi hawatamuachia afanye mambo fulani fulani hivi. Pia na Mandela makaburu walifikiria hivyo. Ni akili za kikoloni tuu hizo, inafurahisha kuona Tanganyika iliokuwa ikijinata kupigania uhuru barani Afrika sasa imekuwa mkoloni na raia wake wengi wakifurahia. Tukumbushe mkuki kwa nguruwe!Kwa Sjingo upande Maalim atatangazwa lakini Serikali yake haitaachiwa kufanya yale ambayo itataka kufanya hususani yaliyo kwenye muungano.
Zanzibar ni nchi ina uhuru wa kujiamulia itakavyo, hakuna ukomo. Muungano sio wa kitakatifu lazima uwe na maslahi ya kiuchumi na wazanzibari. Narudia hoja kuu ni uchumi, kuna kila dalili tena za wazi kama uchumi wa Zanzibar umefifia au kufa kutokana na wakoloni wetu kutofahamu tofauti ya uchumi wa Zanzibar na ule wa Tanganyika. Hili tatizo linaenda deep hadi kwenye utungaji wa sera/economic-policies.
Mpelekeeni salamu huyo Dr.Mwinyi, nasikia anasema ameishi maisha ya kawaida kama wazanzibari wengine. Labda nimdokeze tuu, sie wengine hatuoni kama ni kawaida kila baada ya kilomita chache kupita road-blocks! Way far from what we consider it a normal life!