Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Imefika miaka mitatu tangu viongozi wa dunia wajitolee kutimiza moja ya malengo yenye ujasiri mkubwa katika historia ya afya ya umma duniani: kufanikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030. Kufanikisha lengo hili kutamaanisha kila mtu katika kila jamii atapata huduma nafuu za afya, aidha za kuzuia maradhi au kutibu wanapougua.
Hatari ya kushindwa kutimiza ahadi hii ni kubwa mno. Hatuwezi kumaliza umasikini, kuwalinda watu dhidi ya milipuko ya magonjwa, kusonga mbele usawa wa kijinsia, au kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDGs) bila kuongeza kasi ya safari kuelekea huduma za afya kwa wote.
Kwa bahati nzuri, viongozi wa kitaifa wameanza kuchukua hatua madhubuti za kupanua upatikanaji wa huduma za afya. Kama ambavyo mimi na wengine wengi tumegundua, mafanikio yanategemea kushinda changamoto moja kubwa katika sekta ya afya: mbinu zilizogawanyika kupita kiasi katika utoaji wa huduma. Badala ya kushughulikia ugonjwa mmoja baada ya mwingine, tunahitaji kujenga mifumo ambayo itashughulikia mahitaji mbalimbali ya kiafya ya watu kwa pamoja. Kila mwanamke anapaswa kuwa na mtoa huduma anayeaminika katika jamii yake atakayempa huduma za uzazi wa mpango, chanjo za kawaida kwa watoto wake, au tiba ya kisukari kwa ndugu yake mzee.
Njia bora kwa nchi kufanikisha mbinu shirikishi zaidi ni kuimarisha huduma za msingi za afya, ambazo ndizo mara nyingi ni mlango wa kwanza wa wananchi kuingia kwenye mfumo wa afya. Watoa huduma za afya ya msingi wanaweza kushughulikia zaidi ya asilimia 80 ya mahitaji ya afya. Na kwa kuwa huduma hizi zinatolewa kwa matajiri na maskini sawasawa, ndizo msingi wa jamii yenye usawa na haki.
Kwanza, tunahitaji kudumisha nia ya kisiasa ya kuimarisha huduma za msingi na kufanikisha huduma za afya kwa wote. Kwa muktadha huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amewataka hivi karibuni marais na mawaziri wakuu kuchukua hatua madhubuti za mageuzi kuanzia mwaka huu.
Ninapoanza kuwafikia viongozi wa Kiafrika mmoja baada ya mwingine, natarajia siku tutakapofanikisha huduma za afya kwa wote kwa watu bilioni 7.7 duniani.
Kutokana na uzoefu wangu kama Rais mstaafu wa Tanzania, najua kwamba uongozi thabiti wa ngazi ya juu unahitajika kuendesha mashine ngumu ya serikali. Ndiyo maana niliungana na shirika la utetezi wa afya, Access Challenge, kuzindua kampeni ya “One by One: Target 2030” pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka huu.
Kama sehemu ya kampeni hii, nitakutana na viongozi kote barani Afrika kuwahimiza wachukue hatua za dhati katika kuimarisha huduma za msingi. Lengo ni kulinda haki ya msingi ya afya kwa kila mtoto, kijana, mama na familia.
Viongozi wa kitaifa na wataalam wa afya ya umma wanapaswa kufahamu yote haya na zaidi ili kubaini udhaifu katika mfumo wa huduma za msingi na kuelekeza maeneo yanayohitaji kuboreshwa. Takwimu pia ni nyenzo muhimu kwa wanaharakati wa afya na wananchi wa kawaida wanaotaka kufuatilia maendeleo kwa muda, kuwawajibisha viongozi, na kudai huduma wanazohitaji na wanazostahili. Hata hivyo, mara nyingi ukusanyaji wa takwimu, licha ya uwezo wake wa kuchochea maendeleo na uwajibikaji, unachukuliwa kama jambo la pembeni.
Primary Health Care Performance Initiative (PHCPI) inashughulikia suala hili moja kwa moja. Katika Mkutano wa Kimataifa wa Huduma za Afya za Msingi, PHCPI iliungana na nchi kadhaa duniani kuzindua nyenzo mpya ya kuwasaidia watunga sera na watoa huduma kuboresha afya. Kupitia Vital Signs Profiles, wanaweza kupata taarifa kuhusu huduma za msingi ambazo ni rahisi kuelewa na kutumia.
Ninapoanza kuwafikia viongozi wa Kiafrika mmoja baada ya mwingine, natarajia siku tutakapofanikisha huduma za afya kwa wote kwa watu bilioni 7.7 duniani. Kwa kujitolea kisiasa kwa ngazi ya juu na nyenzo mpya za kukuza upatikanaji wa huduma na kuimarisha uwajibikaji, nina uhakika kwamba tunaweza kufanikisha dira hii yenye ujasiri.
Hatari ya kushindwa kutimiza ahadi hii ni kubwa mno. Hatuwezi kumaliza umasikini, kuwalinda watu dhidi ya milipuko ya magonjwa, kusonga mbele usawa wa kijinsia, au kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDGs) bila kuongeza kasi ya safari kuelekea huduma za afya kwa wote.
Kwa bahati nzuri, viongozi wa kitaifa wameanza kuchukua hatua madhubuti za kupanua upatikanaji wa huduma za afya. Kama ambavyo mimi na wengine wengi tumegundua, mafanikio yanategemea kushinda changamoto moja kubwa katika sekta ya afya: mbinu zilizogawanyika kupita kiasi katika utoaji wa huduma. Badala ya kushughulikia ugonjwa mmoja baada ya mwingine, tunahitaji kujenga mifumo ambayo itashughulikia mahitaji mbalimbali ya kiafya ya watu kwa pamoja. Kila mwanamke anapaswa kuwa na mtoa huduma anayeaminika katika jamii yake atakayempa huduma za uzazi wa mpango, chanjo za kawaida kwa watoto wake, au tiba ya kisukari kwa ndugu yake mzee.
Njia bora kwa nchi kufanikisha mbinu shirikishi zaidi ni kuimarisha huduma za msingi za afya, ambazo ndizo mara nyingi ni mlango wa kwanza wa wananchi kuingia kwenye mfumo wa afya. Watoa huduma za afya ya msingi wanaweza kushughulikia zaidi ya asilimia 80 ya mahitaji ya afya. Na kwa kuwa huduma hizi zinatolewa kwa matajiri na maskini sawasawa, ndizo msingi wa jamii yenye usawa na haki.
Jinsi ya kuimarisha huduma za msingi za afya
Baada ya kutambua faida hizi, viongozi wa dunia walikutana hivi karibuni kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Huduma za Afya za Msingi mjini Astana, Kazakhstan, na kuridhia tamko jipya linalowajumuisha kuimarisha mifumo ya huduma za msingi katika nchi zao. Lakini sasa ndipo kazi ngumu inaanza. Viongozi wa kitaifa wanapofikiria jinsi bora ya kutekeleza ahadi yao, napenda kusisitiza mambo mawili muhimu katika kufanikisha maendeleo.Kwanza, tunahitaji kudumisha nia ya kisiasa ya kuimarisha huduma za msingi na kufanikisha huduma za afya kwa wote. Kwa muktadha huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, amewataka hivi karibuni marais na mawaziri wakuu kuchukua hatua madhubuti za mageuzi kuanzia mwaka huu.
Ninapoanza kuwafikia viongozi wa Kiafrika mmoja baada ya mwingine, natarajia siku tutakapofanikisha huduma za afya kwa wote kwa watu bilioni 7.7 duniani.
Kutokana na uzoefu wangu kama Rais mstaafu wa Tanzania, najua kwamba uongozi thabiti wa ngazi ya juu unahitajika kuendesha mashine ngumu ya serikali. Ndiyo maana niliungana na shirika la utetezi wa afya, Access Challenge, kuzindua kampeni ya “One by One: Target 2030” pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka huu.
Kama sehemu ya kampeni hii, nitakutana na viongozi kote barani Afrika kuwahimiza wachukue hatua za dhati katika kuimarisha huduma za msingi. Lengo ni kulinda haki ya msingi ya afya kwa kila mtoto, kijana, mama na familia.
Mbinu inayotegemea takwimu
Jambo la pili muhimu katika maendeleo ni kuboresha takwimu ili tuweze kufuatilia yale tuliyofanikisha na kubaini kazi iliyosalia. Takwimu sahihi zinahitajika ili kujua kama watu wanakutana na vikwazo vya kifedha au kijiografia katika kupata huduma; kama huduma zinatolewa kwa usalama na ufanisi; na kama zinawafikia makundi yaliyoko pembezoni mwa jamii.Viongozi wa kitaifa na wataalam wa afya ya umma wanapaswa kufahamu yote haya na zaidi ili kubaini udhaifu katika mfumo wa huduma za msingi na kuelekeza maeneo yanayohitaji kuboreshwa. Takwimu pia ni nyenzo muhimu kwa wanaharakati wa afya na wananchi wa kawaida wanaotaka kufuatilia maendeleo kwa muda, kuwawajibisha viongozi, na kudai huduma wanazohitaji na wanazostahili. Hata hivyo, mara nyingi ukusanyaji wa takwimu, licha ya uwezo wake wa kuchochea maendeleo na uwajibikaji, unachukuliwa kama jambo la pembeni.