Mtoa Taarifa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2024
- 213
- 671
Mwenendo wa Bei za Mafuta nchini kwa kipindi cha Miaka 10 (2014-2024 zinaonesha miaka ya 2015, 2016, 2017 na 2020 pekee ndio ilishuhudia Bei za chini za Mafuta nchini Tanzania kulinganisha na miaka mingine
Kwa mujibu wa takimu za EWURA, kwa kipindi cha miaka mitatu (2022, 2023, 2024) bei ya mafuta imebaki kuwa juu kuliko kipindi kingine ikitoka katika Wastani wa Tsh. 2,969 kwa lita hadi Tsh. 3,140 kwa Petroli
Aidha, Septemba 2020, Tsh. 10,000 ilikuwa na uwezo wa kununua Lita 5.3 za Petroli kwa Dar, wakati hadi Septemba 2024, kiasi hicho kinanunua Lita 3.1 za Petroli, Lita 3.3 za Dizeli na Lita 3.2 za Mafuta ya Taa.
Mwenendo wa Bei za Mafuta nchini Tanzania kwa Miaka 10
Mwaka | Petroli | Dizeli | Mafuta ya Taa
2014 - Tsh. 2,267 - Tsh. 2,091 - Tsh. 2,040
2015 - 2,153 - 1,832 - 1,770
2016 - 1,840 - 1,747 - 1,673
2017 - 1,989 1,887 1,811
2018 - 2,373 2,273 2,247
2019 - 2,236 2,168 2,132
2020 - 1,852 1,793 1,692
2021 - 2,427 2,251 2,176
2022 - 2,969 3,125 3,335
2023 - 3,213 3,259 2,943
2024 - 3,140 3,011 3,121
SOURCE: EWURA