Mwaka 2023, wakenya milioni 12 walisafiri kwa ndege ilhali watanzania milioni 3.8. Je, sisi watanzania shida ni umaskini au tunaogopa kusafiri?

Maswali mengine mtu anauliza utafikiri ni mgeni.., Unajua kabisa disposable income kwa waafrika ni tatizo hata Kenya hao wanaosafiri ni kina Ruto, Kenyatta and Moi's et al Na mabwanyeye wengine ila majority hata milo mitatu tatizo... Kwahio unless haya maswali mnaulizana huko na walamba asali mkiwa Monaco au Dubai hapa tungekuwa tunaulizana na vipi watu hatuna maji safi, umeme / nishati ni gharama na hata affordable housing bado sio affordable
 
Upumbavu mtupu, asahivi bongo ni zaidi ya ulaya tujitahidi kutumia fursa anazozitengeneza Mama
 
katika hao Watanzania million 3 wanaopanda ndege, utakuta 90% wa Kariakoo.

Kariakoo ndiyo chimbuko la kila kitu Tanzania hii.
Ninachojua mimi wakina Chief Marealle, Nyerere na Oscar Kambona ni Watanzania wa mwanzo kabisa kupanda ndege kwenda Ulaya na Marekani.
 
Wanasafiri kwenda kuwa mabeki 3 huko Gulf
 
Mbona kama unanitukana Choice variable maana mimi Mwenyewe sijawahi kupanda ndege wala kuona tiketi ya ndege japo nilikuwaga nakwenda pale airport ya Mbeya kabla ya kuihamisha ,kuangalia ndege inapopaa na kushuka😀😀😀
 
Na mlinunuliwa ndege ili msafiri mkasema haziwafai sasa vp kama singenunuliwa hata hzo ndege, tulieni wengi wenu bado hamjtambui ndege mnaona kama anasa.
 
Ww umesafiri mara ngapi
 
Kina Ruto, Moi, Kenyatta wanafika 12M??? Ulianza vizuri kwa kutaja disposable income. Ungemalizia kwa kukiri hadharani Kenya disposable income ipo juu na kuna diaspora wengi zaidi ya TZ. Leta takwimu za diaspora remittances for the 2 countries tulinganishe.
 
Moja kina Ruto Moi et al inamaanisha the 1 per-centers (the walamba asali) na kwa Kenya kuna tycoons na kuna paupers wa kutupa by the way hio research imeweka individuals waliosafiri (unique people) au mara ngapi watu wamesafiri ? (huenda ni watu elfu kadhaa ambao kila wiki wanakwenda kudai kufanya uchuuzi....

Afrika hatuchekani sana kwa majority kutokuwa na disposable income ingawa ofcourse pesa yao ipo juu kuliko yetu...

Kwahio nasimamia point yangu palepale as far as umasikini hatuchekani tena huenda kule kuna mafukara kuliko huku na kipimo cha safari / kusafiri haimaanishi utajiri...
 
Swali zuri sana umeuliza
 
Ulilipiwa na ndugu zako, serikali ya Nyerere au Wagalatia wenyewe wa Canada ulipoenda kusoma kwao??
siyo ndugu yangu, mzazi wangu.

Kariakoo hatujaanza kupanda ndege leo wala jana, tumekuta wazazi wetu wanapanda tayari na siyo kitu cha ajabu.
 
Usafiri wa barabara mzuri ,

Unaweza weka kituo ,

Ukafanya mengine ,

Inapendeza zaidi.
 
Upande ndege uende wapi?… Watu wana roho za kukunjianiana kutoka ngazi ya juu hadi ya chini, Passport tu tunaambiwa ni haki yetu lakini ukianza kufuatilia utazima fegi kwa hivyo vigingi utavyowekewa na hao wadau wanaosimamia hizo secta.

Ikifika time itokee kuna sehemu wanabasilishana uraia na western nam’badilishia mtu nampa na mtaji
 
siyo ndugu yangu, mzazi wangu.

Kariakoo hatujaanza kupanda ndege leo wala jana, tumekuta wazazi wetu wanapanda tayari na siyo kitu cha ajabu.
Kumbe, nilifikiri wengi wenu mlifika nje kwa stowaway tu kwenye meli za Wagiriki😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…