Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Nimeona agenda ya kuftarisha imepamba Moto kila Kona huku majina ya viongozi yakitumika....kila kiongozi akiftarisha anamtaja mwenye nchi unajiuliza hizi fedha wametoa wapi? Je NI kweli wametumwa na wanayemtaja? Au uchawa unawasumbua Hadi kwenye Imani?
Lakini pia ifta ilipaswa iwe Kwa maskini na wale wasio na chakula au futari lakini unashangaa wote wanaoonekana kwenye TV wanajiweza na wameacha misosi kwao. Najiuliza hii inatafsiri gani kidini? Hakuna kiongozi aliyefuturisha ambaye tumemwona akiwa na maskini mitaani wote wanakula kwenye hekalu na kumbi Nono.
Mwisho najiuliza ni lazima ukiwalisha watu chakula uite vyombo vya habari? Wakuu WA wilaya na Mikoa pamoja na wabunge mmefanya siasa kwenye ibada ya mwaka huu; najiuliza mwakani kuelekea uchaguzi mtafanya vihoja gani mwezi mtukufu?
Kuna baadhi ya watu wamefanya mwezi mtukufu uonekane kama mwezi wakuonyesha nguvu ya kisiasa na kiuchumi kwenye kulisha matajiri........mlijisahau mkawaacha walengwa ambao ni wasio na vyakula......mmetumia muda mwingi kualikana Kwa hadhi zenu kwenye jamii.....siyo Jambo jema limewakera wengi