Mwaka Mmoja Na Samia: Kufunguliwa kwa Magazeti Makubwa manne

Mwaka Mmoja Na Samia: Kufunguliwa kwa Magazeti Makubwa manne

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
"Siku chache zilizopita, niliona Mhe. Nape anatoa leseni kwa magazeti manne, magazeti ambayo yalifungiwa kifungo ambacho hakijulikana kingeisha lini. Ndani ya siku 365, tuna kumbukumbu ya kufunguliwa kwa magazeti manne." - Nevile Meena

#MamaYukoKazini
#MwakaMmojaNaSamia

20220319_100817.jpg
 
Katika kipindi chake mwaka mmoja akiwa kama Rais, SSH amejipambanua kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi. Ni kiongozi wenye kushaurika, msikivu, huruma, hofu ya Mungu wake, kutumia lugha ya staha, kupenda amani na maelewano, na pia asiyependa kutumia mabavu na kuendekeza ukanda na udini.

Tofauti na mtangulizi wake JPM, yeye alikuwa ni mtawala juu ya watu, ambaye alitumia utisho wa vyombo vya dola ili apate kutisha na kutiisha (terrifying and subjugating) wananchi na hasa washindani na wapinzani wake. Aliendekeza sana ukanda na ukabila, na hata kuonyesha chuki za wazi kwa baadhi ya makabila na matajiri.
 
Magazeti yenyewe yanaishia kusifia tu hakuna uandishi wenye tija.

Yaani ukiangalia vichwa vya habari vya magazeti karibia kumi yote yana fanana sioni umuhimu wa kuongeza mengine kufanya jambo lilelile.
 
Waziri hapaswi kuwa na mamlaka ya kufunga na kufungulia magazeti. Hili ni jambo liliposwa kuwa la mahakama.
"Siku chache zilizopita, niliona Mhe. Nape anatoa leseni kwa magazeti manne, magazeti ambayo yalifungiwa kifungo ambacho hakijulikana kingeisha lini. Ndani ya siku 365, tuna kumbukumbu ya kufunguliwa kwa magazeti manne." - Nevile Meena

#MamaYukoKazini
#MwakaMmojaNaSamia

View attachment 2156316
 
Back
Top Bottom