Katika kipindi chake mwaka mmoja akiwa kama Rais, SSH amejipambanua kuwa yeye ni kiongozi wa wananchi. Ni kiongozi wenye kushaurika, msikivu, huruma, hofu ya Mungu wake, kutumia lugha ya staha, kupenda amani na maelewano, na pia asiyependa kutumia mabavu na kuendekeza ukanda na udini.
Tofauti na mtangulizi wake JPM, yeye alikuwa ni mtawala juu ya watu, ambaye alitumia utisho wa vyombo vya dola ili apate kutisha na kutiisha (terrifying and subjugating) wananchi na hasa washindani na wapinzani wake. Aliendekeza sana ukanda na ukabila, na hata kuonyesha chuki za wazi kwa baadhi ya makabila na matajiri.