Mwaka mmoja wa Biden madarakani, amefeli vibaya sana

Mwaka mmoja wa Biden madarakani, amefeli vibaya sana

Cathelin

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
2,071
Reaction score
3,995
Biden alijinasibu na kutoa ahadi kemkemu na kumtupia lawama lukuki Trump

Ndani ya mwaka mmoja wa Biden, vifo vya Covid-19 marekani vimezidi vifo vilivyoripotiwa chini ya Trump, wakati Biden kakuta kila kitu,Chanjo, instruments na wamarekani washakuwa na ufahamu wa Covid-19.

Mmfumko wa bei kupindukia, mfumko wa Bei nchini marekani chini ya Biden ni mkubwa toka miaka 40 iliyopiita.

Kukumbwa na uhaba wa gesi na mafuta, Trump aliifanya marekani kuwa Energy independent, lakini Biden kahalibu zaidi, mpaka kutoa reserve ya mafuta ili kusawazisha Bei ya mafuta nchini umo.

Ameshindwa kizibiti uhamiaji, marekani chini ya Biden imeshuhudia uhamiaji haramu ukiongezeka, tofauti na kipindi Cha Trump, kitendo Biden kufungua mipaka kimewaudhi sana wamarekani.

Jinsi alivyojitoa Afghanistan ni kituko Cha karne, alisababisha vifo vya wanajeshi 13 kwa uzembe kabisa, wakati Trump alikuwa ashafanya makubaliano na Turban jinsi ya kujitoa, na katika makubaliano hayo hakuna mwanajeshi wa marekani alikufa Afghanistan ndani ya miezi 18.

Turufu waliobaki nayo Democrats ni tukio la January 06, Ila na Trump amewajibu kwa kishindo, alipokuwa Arizona, alijaza watu hadi Democrats wakapanic.

2024 Trump au Dessantis lazima mmoja atashinda uraisi
 
Biden na Kamara wote wana uwezo wa kawaida. Biden alikuwa kiongozi mzuri miaka ya 90s ila umri kidogo unamtupa mkono kwa sasa. Kamara hana maajabu

Trump umri umeenda sidhani kama atarudi tena kugombea
 
Buden na Kamara wote wana uwezo wa kawaida. Biden alikuwa kiongozi mzuri miaka ya 90s ila umri kidogo unamtupa mkono kwa sasa. Kamara hana maajabu

Trump umri umeenda sidhani kama atarudi tena kugombea
We jamaa, yaani Biden amepata uraisi akiwa na 78, 2024 Trump naye atakuwa na 78, Spika Nancy kana 81 na bado kapo,kwenye Republicans hakuna wa mshinda Trump, uliona ya Arizona
 
We jamaa, yaani Biden amepata uraisi akiwa na 78, 2024 Trump naye atakuwa na 78, Spika Nancy kana 81 na bado kapo,kwenye Republicans hakuna wa mshinda Trump, uliona ya Arizona
Biden umri umemtupa na sio mtu wa kuzeeka vizuri. Katafute clip zake miaka ya 80s na 90s anawashutumu makaburu na kutetea hoja kadhaa uone uongeaji wake halisi. Kwa sasa uwezo umeshuka sana tu. Umri unamchangia kuwa na udhaifu kiutendaji.

Trump na vile vipimo alivyokuwa anafanyishwa kwa mashaka sio mtu wa kumtegemea agombee na miaka 84. Trump ni overweight, anazeeka na kasi
 
Biden alijinasibu na kutoa ahadi kemkemu na kumtupia lawama lukuki Trump

Ndani ya mwaka mmoja wa Biden, vifo vya Covid-19 marekani vimezidi vifo vilivyoripotiwa chini ya Trump, wakati Biden kakuta kila kitu,Chanjo, instruments na wamarekani washakuwa na ufahamu wa Covid-19...
Ana approval rate kubwa kuliko trump unasemaje amefail
 
Biden umri umemtupa na sio mtu wa kuzeeka vizuri. Katafute clip zake miaka ya 80s na 90s anawashutumu makaburu na kutetea hoja kadhaa uone uongeaji wake halisi. Kwa sasa uwezo umeshuka sana tu. Umri unamchangia kuwa na udhaifu kiutendaji.

Trump na vile vipimo alivyokuwa anafanyishwa kwa mashaka sio mtu wa kumtegemea agombee na miaka 84. Trump ni overweight, anazeeka na kasi
Lakin Trump ndo leading Republican contender kwa 2024
 
Back
Top Bottom