Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Umejiajiri kwenye nini?
 
Wewe ni mbinafsi , Afrika haiendelei kwasababu ya fikra binafsi kama hizi , unadhani serikali inao uwezo wa kulipa raia wote hio milioni moja , Kama umepata hio ajira ya milioni moja mshukuru Mungu...Vijana na tujiajiri na tusikate tamaa pale mambo yanapokuwa magumu , akili za kizee kama hizi ngoja zisubirie kiinua mgongo.
 
Ukitaka pesa lazima utumwe na anayekupa, iwe umeajiriwa au umejiajiri.

Biashara na ujasiriamali sio wa kila mtu. Kiuhalisia biashara na ujasiriamali unahitaji watu wasiozidi 20% ya wanajamii kwa eneo lolote.

Kwa Tanzania tatizo sio uhaba wa ajira, tatizo ni uhaba wa fedha unaofanya watu binafsi na serikali wasiajiri/kutoa ajira mpya.

Kujiajiri ni kujiongezea mzigo wa matatizo tofauti na wengi wanavyodhani. Mtu aliyeajiriwa yeye anakula shushu tu na mshahara unaingia.

Ukijiajiri unaweza kujikuta unafanyakazi kwa hadi 18hrs kwa siku tofauti na aliyeajiriwa ambaye yeye ni 8 - 10 hrs kwa siku. Awe kazalisha au hajazalisha yeyehilo halimhusu.
 
Aisee[emoji706][emoji706][emoji706]
 
Huu ni ukweli, tatizo wengi hawapendi kuusikia ukweli.
 
Kama umeipanga timu yako vizuri, hakuna shida; wewe mmiliki hautahusika moja kwa moja kwenye uzalishaji, bali watu uliowaajiri ndio watakufanyia uzalishaji.
 
Jobless umepanic 😂😂
 
Nchi haiendelei kwa watu kujiajira, hapa nakukatalia kabisa. Nchi inaendelea kwa watu wake kuacha uvivu, kuwa wabunifu na kuwa wagunduzi mambo mbali mbali hasa ya kisayansi na teknolojia.

Watu wanaweza wakawa waajiriwa popote na nchi ikaendelea ilimradi tu waache uvivu, wawe wabunifu na wagundue mambo mbali mbali.

Hayo mengine ni visingizio tu.
 
Sekta binafsi(waliojiajiri) ndio inayoleta ugunduzi na uvumbuzi; kuajiriwa kwako umevumbua nini kiteknolojia?
 
Sekta binafsi(waliojiajiri) ndio inayoleta ugunduzi na uvumbuzi; kuajiriwa kwako umevumbua nini kiteknolojia?
Nani kakwambia nimeajiriwa Mkuu? Au umejiamulia kuja na conclusion yako?.

Unakosea sana unaposema waliojiajiri ndio wagunduzi, huu ni ujinga wa hali ya juu Mkuu.

Mtu yoyote anayefanyakazi kwa bidii anayetaka maendeleo haijalishi ameajiriwa au kajiajiri anaweza kuwa mgunduzi.

Hivi unajua utofauti wa kuajiriwa sekta binafsi na serikalini ni ndogo sana na ambayo haiathiri ugunduzi wa mtu.

Tatizo sisi vijana wa kitanzania ni wavivu sana na walalamishi mno.
 
Wengine wanafikiri kufanya biashara unahitaji akili ya shule kama degrees au uwe na mtaji mkubwa sana wa kuanzia biashara

Babu yangu hakusoma kabisa ila kwenye kurudisha chenji na kuendeleza mtaji alikuwa makini sana mpaka kumfundisha na mwanae (baba)
Leo biashara zinaendelezwa na wajukuu
Kuna mzee alikuwa anahojiwa biashara zao zilianza 1930s na 40s na sasa warithi wanakuja ila waendeleze
 
Kama umeipanga timu yako vizuri, hakuna shida; wewe mmiliki hautahusika moja kwa moja kwenye uzalishaji, bali watu uliowaajiri ndio watakufanyia uzalishaji.
Shida ya mbongo inakuwa hapa akisikia neno kujiajiri anafikiria ujasiriamali.

Wewe ni mwanasheria umefanya kazi ya kuajiriwa umekusanya pesa ya kutosha kwanini usiache ajira na kuanzisha Law firm yako, wewe Ni daktari ushajijengea jina watu wakakuamini kwanini usifungua kliniki yako na mdogo mdogo ikawa hospitali ukaajiri watu wengi , Wewe ni mhasibu na CPA yako kuliko kuendelea kuajiriwa kwanini usitoke kwenye comfrot zone na kuanzisha Auditing firm yako.
Kama raia tukiwa na mawazo haya nchi itapiga hatua, maana faida zake ni nyingi kwanza utaacha nafasi ya watu wengine kuajiriwa na wewe pia utaajiri , kuliko kusubiria kufa au kustaafu ili wengine wapate ajira.

Nchi ya Marekani yenye idadi ya watu zaidi ya milioni 150 ni asilimia 18 tu ya idadi yote ya watu wameajiriwa serikalini na asilimia zote zilizobaki ni sekta binafsi na wengine kujiajiri.
Maana yake ni nini? , hata taifa kibwa kama Marekani halina uwezo wa kuajiri raia wake wote sasa Sembuse Tanzania ambayo ndio kwanza hata uchumi wa kati hatujafikia.

Ukishajiajiri na ukatoboa maana yake unaingiza biashara yako au Kampuni yako katika orodha ya sekta binafsi.

Wenzetu wamepiga hatua kwasasabu mitazamo yao ishabadilika muda mrefu lakini sisi ndio kwanza tunalumbana hapa kitu ambacho kipo wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…