Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Tunaamini elimu tunayoipata huko vyuoni na mashuleni, inatupa uhuru wa kufanya maamuzi sahihi katika uzalishaji mali pamoja na kujitegemea.

Tulitegemea ujuzi na elimu ulioipata huko duniani n.k iwe chachu ya wewe kujijenga na kuanzisha na kumiliki kampuni, taasisi, au kiwanda ili pia iweze kutoa ajira kwa wengine.

Mtaji kwako sio tatizo, kwa sababu umeshaajiriwa kwa miaka mingi na una sifa zote za kukopa; Swali, kwanini unashindwa kujiajiri?

Tatizo ni nini?​
Kwanza hakuna sehemu yeyote Duniani ambako kila mtu anaweza kujiajiri,Ili uzalishaji afanye nani Sasa?
 
Kwa sisi waTz weusi hawa ni 99%
Watu wengi wana Illusion kwenye suala la kujiajiri na mwisho wa siku waanzisha tuvitu tudogo tudogo ambavyo sio sustainable.

Biashara nyingi sana za kujiajiri nilizoziona hapa Tanzania kwetu ni za kiulanguzi na sio za uzalishaji na hazina sustainability.

mfano watu waliojiajiri maduka ya nguo Kariakoo mwaka 2024, yaani internet inakuwa lakini bado wao hawajaona hili.

Kingine huwezi kufanikiwa kwenye biashara kama huwezi hukufanikiwa kwenye ajira, kama huna nidhamu, matumizi ya mabaya ya pesa usikurupuke kujiajiri
 
Kujiajillri inahitaji Uthubutu kwa kuwa njia yake sio rahisi na matokeo yake ni ya mda mrefu.

Binadamu hatufafanani, Suala la Uthubutu sio la kila mtu, Dunia yote inafahamu hilo.
Ni kweli matokeo ya kujiajiri ni ya muda mrefu, na wengi tunashindwa kwa kutaka matokeo ya muda mfupi
 
Hata biashara hatuwezi kufanya wote kwa namna yeyote ile, hata tukifanya watu wengi watafeli.

Walioajiriwa kupitia mishahara ,posho ndio wanaongeza mzunguko wa pesa mitaani kwa wafanyabiashara.
Na waliojiajiri walikuwa wanawaza hivi kweli?
 
Biashara nyingi sana za kujiajiri nilizoziona hapa Tanzania kwetu ni za kiulanguzi na sio za uzalishaji na hazina sustainability.
Ni kweli kutegemea biashara ya ulanguzi katika kujiajiri ni ngumu; ila kwa yule aliyewekeza kwenye mashine/mitambo ya uzalishaji huyu ni rahisi kujiajiri kwa sababu anatengeneza na kuuza.
Lakini wapo watu wenye hiyo mitaji, kwa nini hawafanyi; tatizo ni nini, elimu au uwoga?​
 
Unaruhusiwa kutoa maoni yako, kwa nini hatujiajiri huku mtaji ukiwa si tatizo?
Kujiajiri kiukweli ni kuajiriwa na wateja wako!! Wateja ni wafalme!! Utalaziomika kuwasikiliza na kuteleleza wanayotaka!! Kiuhalisia ni kwamba kujiajiri ni kuajiriwa na wateja!! Wateja ndo mabosi na waajiri wako!! You are not free!!
 
Back
Top Bottom