Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Wataalam wa uchumi waje watuambie kama inawezekana kila mtu kujiajiri, uchumi utakua sawa kweli?

Nataka kujua
Iko hivi:
Sio kila mtu anaweza kujiajiri, lazima wengine waajiriwe na wengine wajiajiri na hii sio dhambi ila nadharia za kiuchumi, ndio kusema sector binafsi na ajira za kuajiriwa zinategemeana.


Ila kiufundi ajira binafsi zikiwa nyingi ambazo ni formal kwa maana zinaeleweka kwenye kulipa kodi, uchumi hukua. Ikumbukwe kua hata wewe ukijiajiri lazima utaajiri watu.
 
Kuna mwaka nilijipanga kununua flat screen mpya ya nyumbani. Nikaingia mtandaoni na kuongea na muuza mali kwa njia ya simu. Akanielekeza mpaka dukani nikafika. Nikapokelewa na kijana wa kiarabu nahisi alikuwa O level. Kilikuwa kipindi cha likizo za shule. Akanipeleka kwenye sectiona ya flat screen kwenye duka na kunipa kila sifa ya TV iliokuwa mbele ya macho yangu. Mimi nilikuwa na ingia google na kuandika model namba ya TV na specs zake zipo kama dogo alivyosema. Nilikuwa na budget ya 1M, ila dogo kanishawishi kununua TV ya 1.5 M yenyewe warranty ya miaka 2. Kaniitia mtu wa usafiri na bei kambana na kumshusha. Mali ilifika salama na haijapata tatizo lolote huu mwaka ushapita. Baada ya siku kadhaa ya kununua ile TV, nilipigiwa simu na yule dogo na aliniulizia ufanisi ya TV.

Wenzetu biashara wana wazoesha watoto wao tangia mashuleni. Wakati sisi waswahili kipindi cha likizo tukienda tuisheni mchikichini ili kupanga mabanda mitihani ya taifa. Waswahili tukimaliza vyuoni ndo tuna tembeza CVs na mavyeti.

Na bado hatujashtuka!
Doh..

Mkuu umeongea ukweli,kuna jamaa mmoja ni muhindi pale uhuru yupo dukani na babake aisee ukienda dukani kwao anakupa somo kuhusu bidhaa zao na kila kitu na kama kuna bidhaa hapo dukani kwao haina sifa anakwambia yaani unaona kabisa hana tamaa utakachoangalia mwisho wa siku ni thamani ya pesa yako ubebe bidhaa ipi.

Automatically nimekuwa wakala wa duka lao ili kukwepa lawama kwa ndugu na jamaa pindi wanaponihitaji niwasaidie kununua au kupata bidhaa kutoka kkoo.
 
Wote tukijiajiri nani ataajiriwa?
Elimu tunayoipata ndio inatufanya tuwaze hivyo, haitufanyi kujiamini na kufanya maamuzi magumu ya kufanya vitu tofauti tofauti katika uwekezaji wa viwanda pamoja na kujiajiri.
 
Wee fala nini unajua utamu wa kuajiriwa tena serikalini..?
No pressure full job security na uhakika wa mshahara na allowance za hapa na pale...
Kujiajiri ni kipaji kama ilivyo football au mziki
Nilijua lazima cheap labour waje kwa kishindo; kujiajiri ni zaidi ya kupata pesa tu; ndio maana nasema inawezekana namna tunavyowaza inaweza kusababishwa na namna tulivyozaliwa au elimu tunazozipata duniani ndio zinazotuathiri.
 
Kabisa kuajiriwa ni rahisi. Wewe unasubiri mshahara tu mwisho wa mwezi hujali kama kuna hasara au faida.
Hivi mada ilikuwa kipi ni rahisi kati ya kuajiriwa na kujiajiri? Sikujua hilo.
No, hii concept ya kutumwatumwa ni kama ilichukuliwa ni tatizo, anyway haya mambo ya kuajiriwa na kujiajiri naona kama huwa yanaongelewa kinadharia sana kuliko kiuhalisia
 
No, hii concept ya kutumwatumwa ni kama ilichukuliwa ni tatizo, anyway haya mambo ya kuajiriwa na kujiajiri naona kama huwa yanaongelewa kinadharia sana kuliko kiuhalisia
Anyway kila mtu anafanya kile anachoona kinamnufaisha.
Mwingine anapenda kujiajiri na hustle zake, mwingine anaona hustle za nini wacha niajiriwe mwisho wa mwezi nachukua changu
 
Kuna watu wanajiajiri kwenye vitu wakifa na vyenyewe vinakufa.

Also hawana sustainability plans
Hili nalo ni tatizo, lakini wakiwa na misingi mizuri, kizazi mpaka kizazi kitakuwa kwenye hiyo shughuli alioianzisha
 
Back
Top Bottom