amshapopo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 1,834
- 4,161
Wakuu habari za siku nyingi,
Natumai ni wazima wa Afya Allah anazidi kutupigania.
Ni mwaka mwingine unaelekea ukingoni natumai tulijiwekea malengo na vipaumbele mbalimbali, sasa huu ndo Muda muafaka wa kufanya analysis kama yaliyomo yamo au hayamo.
Sijigambi kwa lolote or Chochote. Dunia ni yetu sote kila mtu anauwezo wa kumake ni swala la Muda tu kikubwa kutanguliza nidhamu japo Mimi hiyo nidhamu imeanza kupotea ukilinganisha na mwaka uliopita.
Mwaka huu nimefanikiwa kufanya saving ya 7.8 ml kwa vipato vyangu nivipatavyo. Jambo kubwa nililoamua kujitosa mwaka huu ni kutoa hela zangu UTT 60ml na kutupia hisa za CRDB, niliamua kufumba macho kama liwalo na liwe lakini kwa dalili yajayo yanafurahisha!
Nilijaribu betting kwa tamaa ya kupata hela ndefu, nikapigwa 2m kavukavu. Hapa nilijifunza tamaa mbaya na hakuna pesa ya rahisi
Yote kwa yote mungu mwema! Usiogope kujiwekea akiba kwani hatujui ya mbele na kazi hazina guarantee. Kama ilivyokawaida kipindi kama hichi huwa nafurahia kwa yote mungu aliyonijalia kuyafikia.
Asante