Mwaka wa Yanga huu, kavunja kila aina ya rekodi Kombe la Shirikisho

Mwaka wa Yanga huu, kavunja kila aina ya rekodi Kombe la Shirikisho

Mtanzanias

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1,747
Reaction score
3,725
Kampiga na kumtoa nje ya michuano Mwarabu (Club Africain), hakuna timu Tanzania imewahi kumfunga Mwarabu akiwa kwenye ardhi ya nyumbani kwake ndani ya dk. 90!

Kampiga Rivers nyumbani kwake ambapo alikuwa hajawai kufungwa tokea 2021 kwenye uwanja wake wa nyumbani, tukumbuke na Whydad Casablanca alichezea kichapo pale.

Kampiga TP Mazembe nyumbani kwake akiwa hajapoteza mchezo kwa timu za Tanzania.

Kamkalisha Malumo Gallants nyumbani kwake ambaye hajawai kupoteza mchezo kuanzia hatua ya mwanzo ya Michuano hii ya Shirikisho barani Africa kwenye uwanja wake.

Pamoja na hayo Yanga kavunja rekodi ya kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho barani Africa tokea michuano hii ibadilishwe jina na kuitwa Kombe la Shirikisho, hakuna timu yoyote imefika iyo hatua kwa timu za Africa Mashariki na Kati.

Pamoja na hayo Yanga kavunja rekodi nyingine ya kushinda mechi nyingi ugenini kwenye michuano mikubwa barani Africa, kashinda mechi 4 ugenini jambo ambalo hakuna timu yoyote Tanzania imewahi kufanya hivyo kwenye michuano ya kimataifa! Alimpiga Club Africain, akampiga Rivers, akampiga TP Mazembe, akampiga Malumo Gallants!

Na bado pia ndiyo timu iliyoruhusu magoli machache sana kuliko timu zote zilizoshiriki michuano hii ikiwa imeruhusu magoli 5 tu mpaka kuingia Fainali!

Kwa maana hiyo sitoshangaa kama Kombe hili la Shirikisho litatua kwenye ardhi ya Tanzania. Wako vizuri na wapewe maua yao, wanaiweka Tanzania kwenye ramani nyingine kisoka.🙌🙌🙌🙏🙏🙏
 
Pia isisahau kuwashukuru Al hilal kwa kuwatoa kwenye caf champion league hatua za awali bila hivyo haka kamserereko mnakokapata kwa kukutana na vibonde sizani kama ungevipata kwenye caf champion league ligi ya wanaume
 
Wewe ulishindwa nini kufika ata nusu mwaka jana? Yaani samaki iliyooza inaicheka samaki nzima ni maajabu ya dunia!
 
Pia isisahau kuwashukuru Al hilal kwa kuwatoa kwenye caf champion league hatua za awali bila hivyo haka kamserereko mnakokapata kwa kukutana na vibonde sizani kama ungevipata kwenye caf champion league ligi ya wanaume
Huko si waliwepo kufa kiume fc?
Kwani imekuwaje tena
 
Hakuna Timu ya Tanzania imefika hatua hii ya kombe la washindi ya klabu za Africa isipokuwa Yanga kombe lenye hadhi ya pili baada ya klabu bingwa afrika
 
Back
Top Bottom