Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, ndugu Fredrick Mwakalebela ambaye amefungiwa kutojihusisha na masuala ya soka nchini kwa kipindi cha miaka mitano pamoja na kutozwa faini ya sh. milioni saba, amekiri kufanya makosa na kuiomba radhi TFF kwa yale aliyotamka hadi yakapelekea kupewa adhabu hiyo.
Mwanamichezo huyo amekiri kwamba hata adabu aliyopewa ilizingatia kanuni, na kwamba kila kosa aliloadhibiwa lilitajwa sambamba na adhabu ya kikanuni inayohusika. Mwakalebela amezungumza hayo wakati akifanyiwa mahojiano na mwandishi maarufu wa habari za michezo nchini, Saleh Ally maarufu kama Saleh Jembe wa Global TV
Hatua hii ya Mwakalebela inaweza kutafsiriwa kama kuiweka njia panda klabu yake ya Yanga ambayo iliwahi kutoa taarifa kwa umma kuelezea dhamira yake ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya TFF kwani kwa kufanya hivyo, klabu itakuwa ikiwasilisha malalamiko kwa niaba ya mtuhumiwa ambaye ameshakiri kufanya makosa na kuomba radhi, tena akienda mbali zaidi kwa kuisifia TFF kwa hatua kubwa iliyopiga katika kuupaisha mpira wa miguu katika nchi yetu.