TANZIA Mwakata, Shinyanga: Ajali ya magari matatu 'Lori, IST, Hiace' na Trekta yadaiwa Watu 20 wamefariki, 15 wajeruhiwa (Agosti 8, 2022)

TANZIA Mwakata, Shinyanga: Ajali ya magari matatu 'Lori, IST, Hiace' na Trekta yadaiwa Watu 20 wamefariki, 15 wajeruhiwa (Agosti 8, 2022)

Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama mkoani Shinyanga.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nne usiku Jumatatu Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori/Scania yenye namba za usajili T658 DUW.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hospitali ya Kahama watu 20 wamepoteza maisha na 15 kujeruhiwa katika ajali hiyo na majeruhi wanaendelea kupata matibabu.

"Watu 17 walipoteza maisha papo hapo eneo la tukio na watatu wamefariki baada ya kufikishwa hospitali,majeruhi wapo 15", taarifa inaeleza.

Mpaka sasa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga halijazungumzia kuhusu tukio hili,juhudi za kumtafuta Kamanda wa polisi zinaendelea.
Pole kwa wafiwa na Mungu awasaidie waliojeruhiwa.
 
Kuna vizee vichawi Sana vya haya Mambo, Miaka ya nyuma Kuna kamoja walikaudhi wanakijiji wenzie kakatengeneza mvua ya mawe, mvua ilikuwa kubwa mno haikatiki mpaka wakakafuata nyumbani kwake walikuta kapo na vitendea kazi kanasema "zogo mvula" ,walipokaomba msamaha ikakatika
 
Ila tusisingizie uchawi,huo uzembe umeanzia kwa dereva wa ist imekutwa k-vant kwenye gari pamoja na operator wa tractor nae anamakosa,huyo wa hice ndio kichaa wakutupwa kabisa.Huyu bila shaka alitumia kilevi pia.ALL IN ALL MAY THEIR SOULS REST IN PEACE
 
Pombe sio nzuri wakati waku drive, imewachukua wengi
 
Kama nawaona wabrashi viatu wakishukuru maombi yao kujibiwa. Wangependa ajali kubwa kubwa kumthibitisha Kinana wrong.

Kazi kweli kweli.
Na watarudi barabarani kwa fujo sana safari hiii!!!
 
Back
Top Bottom