Mwakinyo amshinda Mnamibia, Tony Rashid apoteza mkanda kwa Msauzi

Mwakinyo amshinda Mnamibia, Tony Rashid apoteza mkanda kwa Msauzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Hassan Mwakinyo Vs Julius Indongo
Rounds: 12
Winner: Mwakinyo kwa KO
Title: African Boxing Union Super Welter

Stay there! Matokeo yatawekwa yote ya mapambano ya utangulizi hadi main card

Pambano la kwanza la utangulizi
Fighters: Kazumba Vs Ayoub Athuman
Rounds: 6
Winner: Ayoub Athuman kwa KO

Pambano la Pili
Fighters: Abdul Juma Kubira Vs Ally Ngwando
Rounds: 6
Winner: Ally Ngwando kwa Points

Pambano la Tatu (Wanawake)
Fighters: Flora Machela Vs Aisha Kizango
Rounds: 6
Winner: Flora Machela kwa Points

Pambano la nne
Fighters: Haidari Mchanjo Vs Allen Kabungo
Rounds: 8
Winner: Haidari Mchanjo kwa points


Pambano la Tano
Fighters: Adam Lazaro Vs Amanyise Isakwisa Isaya(Manyisa)
Rounds: 8
Winner: Adam Lazaro, KO, Round ya 2

Boughts za Kimataifa

Pambano la Sita (Kimataifa)
Fighters: Tony Rashid(Tz) Vs Bongani Mahlangu(South Afrika)
Rounds: 12
Winner: Bongani, TKO Round ya 12

Tonny Rashid amepoteza mkanda wa African Boxing Union Super Bantam
 
Pambano litakaloleta Sura mpya ya ngumi Tanzania.
Bondia mkali,mzoefu(Julius) na bondia anaechipukia,mwenye nguvu na mvumilivu (Mwakinyo) wanapanda ulingoni.

Kwa mara ya kwanza Mwakinyo anakutana na mpiganaji fundi na mzoefu. Ili Mwakinyo ashinde lazima aingie na mipango imara kwa kila round na aache kupigana kama siku zote.

Mitindo ya upiganaji hua inabadilika kutegemeana na aina ya bondia,urefu na mipango anayojipangia kila bondia anapoingia ulingoni.

Kwa mtazamo wangu..Leo Mwakinyo atakua anaingia kwanza ( be first) na mpinzani wake atatumia back pedal( atakua nashambulia kwa kupiga hatua za nyuma) hii ni kutokana na ufupi wa Mwakinyo dhidi ya mpinzani wake.
Na kwakua wote no Orthodox Stance boxer ..Mwakinyo anatakiwa kufanya kazi ya ziada ya kuingia ndani ili ashambulie na wakati huohuo Indogo anaweza kushambulia kwa mbali na kutumia ngumi yake ndogo (Jab) kumzuia Mwakinyo kuingia huku akipanga mashambulizi.

Ukweli ni kwamba Mwakinyo ana kazi ya ziada ili apate ushindi. Anatakiwa awe na foot speed ya kiwango cha juu ili avunje ukuta na aingie au apige "hook punch" nyingi ili ashushe kimo cha mpinzani wake kisha afanye finishing kwa upper cut punch au cross punch. Mipango hii lazima iwe ndani ya round sita za kwanza na si zaidi na hapo atashinda kwa TKO au KO.. Kinyume na round hzo pambano litakwenda mpk mwisho na uhakika wa Indogo kushinda kwa point utakua mkubwa kwakua Mwakinyo hatoweza kutengeneza point kirahisi lkn pia Indogo atatumia uzoefu wake na urefu wake kuvuta muda kwa kufanya "clinching" za mara kwa mara.

Hata hivyo ngumi ni mchezo wa bahati pia lolote linaweza kutokea.
 
Mwakinyo na huyo mNamibia ngap ngap huko?
 
Back
Top Bottom