Mwakinyo ashikiliwa na Polisi Tanga, akituhumiwa kum-shambulia mtu

Mwakinyo ashikiliwa na Polisi Tanga, akituhumiwa kum-shambulia mtu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini na bingwa wa mkanda wa WBO Afrika katika uzani wa middle, Hassan Mwakinyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga akituhumiwa kum-shambulia mtu anayedaiwa kuingia katika eneo lake bila ya ridhaa yake.

1741355791954.png
Mwakinyo anashikiliwa na jeshi hilo tangu jana Alhamisi katika Kituo cha Chumbageni kutoka-na sakata hilo, huku mtu aliyemshambulia akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga.

Sababu kubwa ya bondia huyo kushikiliwa na jeshi hilo ni kutokana na madai ya kumshambu-lia mtu huyo na kumsababishia majeraha ma-kubwa mwilini.

Mwananchi limemtafuta Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Maket Msangi am-baye amekiri kuwa wanamshikilia bondia huyo maarufu nchini.

"Tunamshikilia Hassan Mwakinyo, hatumshikilii bondia. Hakuna shida ila ana tuhuma za kum-shambulia mtu ambaye inasemekana alipita maeneo ya nyumbani kwake na kujaribu kuin-gia kwa namna ya mazingira ambayo inadaiwa ni kwa nia ya kutenda kosa, kwa hiyo akamka- mata," amesema Msangi.

"Wakati tunapewa taarifa alikuwa amemkamata, polisi tulienda kwa ajili ya kumchukua mtuhumiwa lakini alikuwa kidogo ana majeraha, tukampeleka akapate huduma ya kwanza Bombo kwa hivyo tunamshikilia kutokana na kumkuta mtuhumiwa kidogo ana majeraha, Tunaendelea kumhoji Mwakinyo kwa nini mpaka akajeruhiwa hivyo."

Chanzo:
Mwananchi
 
Hakuna mtu mwenye ruhusa ya kutoa hukumu ya kosa lolote isipokuwa mahakama.
Kwahiyo mwakinyo nae amejichukulia Sheria mkononi Hivyo nae ni mtuhumiwa wa uharifu Tu kama wahalifu wengine.
 
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Hassan Mwakinyo anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa wa Tanga, akituhumiwa kumshambulia mtu anayedaiwa kuingia katika eneo lake bila ridhaa yake.

Mwakinyo anashikiliwa na jeshi hilo tangu jana alhamisi katika kituo cha polisi Chumbageni kutokana na sakata hilo huku mtu aliyemshambulia akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bombo iliyopo Tanga.

Chanzo cha kuaminika kimelieleza gazeti la Mwananchi kuwa sababu kubwa ya bondia huyo kushikiliwa na jeshi hilo ni kutokana madai ya kumshambulia mtu huyo na kumsababishia majeraha makubwa mwilini.

Mwananchi limemtafuta kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, ACP Maket Msangi amekiri pia wanamshikilia bondia huyo.

"Sisi tunamshikilia Hassan Mwakinyo hatumshikilii bondia.
Hakuna shia ila ana tuhuma za kumshambulia mtu ambaye inasemekana alipita katika maeneo ya nyumbani kwake na kujaribu kuingia kwa namna ya mazingira ambayo inadaiwa ni kwa nia ya kutenda kosa kwa hiyo akamkamata," amesema Msangi.

"Wakati tunapewa taarifa alikua amemkamata Polisi tulienda kwaajili ya kumchukua mtuhumiwa lakini alikua kidogo ana majeraha tukampeleka akapate huduma ya kwanza Bombo kwa hivyo tunamshikilia kutokana na kumkuta mtuhumiwa kidogo ana majeraha, Tunaendelea kumhoji Mwakinyo kwanini mpaka akajeruhiwa hivyo.

"Hivyo elewa kwamba tunamshikilia kwasababu hiyo tutafikisha suala hilo ofisi ya mashitaka kwaajili ya kutafsiri sheria na kama kuna tatizo ushahidi unathibitisha kosa basi hatua nyingine stahiki zitachukuliwa," alisema Msangi.
 
Imekuaje Tena,

Mwakinyo si alishasema hapigani Kwa pesa ndogo?

Sasa mbona kapigana mitaani Bure!🤔

Na sio ajabu,
pesa za Hilo pambano anakwenda kuzitoa yeye mwenyewe pale polisi🤔
 
Sisi tunamshikilia Hassan Mwakinyo hatumshikilii bondia.
Hakuna shia ila ana tuhuma za kumshambulia mtu ambaye inasemekana alipita katika maeneo ya nyumbani kwake na kujaribu kuingia kwa namna ya mazingira ambayo inadaiwa ni kwa nia ya kutenda kosa kwa hiyo akamkamata," amesema Msangi.
😅😅
 
Imekuaje Tena,

Mwakinyo si alishasema hapigani Kwa pesa ndogo?

Sasa mbona kapigana mitaani Bure![emoji848]

Na sio ajabu,
pesa za Hilo pambano anakwenda kuzitoa yeye mwenyewe pale polisi[emoji848]
Uwezo wako wa kufikiri ni Mdogo sana.

Kwa maelezo ya Kamanda, kwa lugha nyepesi huyo aliepigwa ni intruder, ambaye Intruder siku zote Nia yake hua ovu. Kwa sababu katika akili yako ya kawaida unawezaje kupita ama kuingia kwenye makazi ya mtu bila ridhaa yake, na zaidi hakujui.
 
Back
Top Bottom