Mwakinyo ashinda kwa TKO dhidi ya muargentina

Mwakinyo ashinda kwa TKO dhidi ya muargentina

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Bondia Hassan Mwakinyo na Jose Carlos Paz wa Argentina Next door arena leo
Mataifa sita, mapambano manne, ulingo mmoja

Bondia Jose Carlos Paz ana rekodi ya kupanda ulingoni mara 35, ameshinda mara 23 ambazo 13 zikiwa ni Kos, amepoteza mara 11, mara 6 kwa Kos na amesuluhu moja

Mwakinyo ni mtanzania ana rekodi ya kupanda ulingoni mara 19 ameshinda mara 17, kati yake 11 alishinda kwa KO pia alipoteza mapambano mawili

Mapambano
1. Zulfa Yusufu Macho(TZ) Vs Alice Mbewe (ZAMBIA)
Rounds: 06
Wieigh: Super Fly weather weight
Winner: Zulfa Macho kwa points

2. HUssein Itaba (TZ) Vs Alexander Kabangu (DRC)
Rounds: 10
Weight: Super Middle Weight
Winner: Alexander Kabangu(Mkongo) maamuzi yalibadilishwa na kusema kuwa ni suluhu

3. Fatuma Zarika (Kenya) Vs Pantiance Mastara(Zimbabwe) Mastara anapigana Southpole Stance
Rounds: 10
Weight: Super Bantam Weight
Winner: Fatuma Zarika

4. Hassan Mwakinyo(TZ) Vs Jose Paz(Argentina)
Rounds: 12
Uzito: Intercontinental Super-welterweight
Winner: MWAKINYO (TKO)

1605301817535.png
1605301868807.png


MAJAJI WACHANGANYANA UAMUZI WA PAMBANO LA MKONGO NA MTANZANIA
-
Mapambano ya Utangulizi la uzito wa kati la round kumi kati ya mtanzania Hussein Itaba na Alexander Kabangu wa DR-Kongo limeonyesha walakini

Baada ya kuisha pambano hilo, Kabangu alitangazwa kuwa mshindi kwa points. Itaba alikataa kushuka ulingoni

Maamuzi yakabadilisha na pambano hilo liliamuliwa kuwa suluhu

Hili lilikuwa pambano la utangulizi kuelekea pambano kuu la Hassan Mwakinyo na Jose Paz
 
Nafuatilia nikiwa kona ya Kilakakala, BEER O'CLOCK
 
Waandaaji wamekula hasara...
Viti vipo wazi wameweka kiingilio vya juu kisa wamepeleka shindano ushuani. Kuna katabia kameibuka hapa bongo kwenye vihoteli , saloon wakirembaremba kidogo huduma unakuwa zajuu sasa na hawa wamejidanganya kuwa watapata watu sasa ona bora wangeweka viingilio vya kawaida
 
Waandaaji wamekula hasara...
Viti vipo wazi wameweka kiingilio vya juu kisa wamepeleka shindano3ushuani. Kuna katarina kameibuka hapa bongo kwenye vihoteli ,saloon wakirembaremba kidogo huduma unakuwa zajuu sasa na hawa wamejidanganya kuwa watapata watu sasa ona bora wangeweka viingilio vya kawaida
Muda bado Sana hapo watu wanaanza kuingia saa nne saa tano
 
Back
Top Bottom