Mwakyembe aitwa na NaCoNGO kueleza kwa kina madai aliyoibua kuhusu baadhi ya ngo kuhusika kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini

Naona wanajitekenya... bora tu Lilian akae kimya... mambo ni magumu mno, they have deep roots in all systems... unless tungekuwa nchi huru
Au amewahi ili asitajwe, na akitajwa ionekane ni siasa?
 
Imeandikwa katika gezeti la NIPASHE:

BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), limeanza kuyahoji mashirika 29 yasiyo ya kiserikali (NGO), dhidi ya tuhuma iliyoibuliwa na Waziri wa zamani, Dk. Harrison Mwakyembe na baadaye kusambaa kwenye mitandao ya kijamii alizodai zinajihusisha na kampeni ya kueneza ushoga nchini.

Mwakyembe ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali ikiwamo Waziri wa Katiba na Sheria, alitoa taarifa hiyo kwenye mkutano ulioandaliwa na viongozi wa dini kupinga mapenzi ya jin-sia moja uliokuwa na kaulimbiu 'Tanzania bila ushoga inawezekana'.

Kwenye taarifa yake, alisema utafiti wal-ioufanya kupitia tume aliyoiunda umebaini kuna mashirika 29 yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na vitendo vya kueneza map-enzi ya jinsia moja (ushoga), jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kitanzania.

Kupitia tamko hilo lililogusa hisia za watu wengi na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamil, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Lilian Badi alisema baada ya kuona taarifa hiyo kuna hatua kadhaa walizichukua kukabiliana na kilichoibuliwa.

“Tumeyaita na kuanza kuyahoji hayo mashirika yaliyotuhumiwa na kufanva uchunguzi wa kina na tunamuhoji Dk. Mwaky-embe ili tujue alifanyaje utafiti wake mpaka akabaini uwapo wa NGOs 29 zinazoshinikiza ushoga."

"Tulifanya kikao cha dharura cha kamati tendaji kujadili namna ya kuchunguza hali hiyo na kuweka maazimio ya utekelezaji, kufanya mawasiliano ya awali na mashirika. yote yaliyotuhumiwa kupitia utafiti huo ikiwa ni maandalizi ya kuwafanyia uchunguzi pamoja na mahojiano ya kina," alisema DK. Lilian na kuongeza

"Hatua nyingine, tumeomba kukutana na kamati ya Dk. Mwakyembe ili tupatiwe taarifa yao itusaidie kuendeleza maoni yetu na juhudi tutakazozichukua kama viongozi wa sekta na NGO."

Alisema baada ya kukamilisha hatua hizo, wataandaa taarifa ya pamoja itakayoambatana na tamko kwa umma kuweka hadharani hatua watakazozichukua.

Alitahadharisha kuwa ni vyema kutambua suala hilo ni mtambuka sio NGO pekee wanaohusika, hata serikali pia kupitia vyombo vyake, wabia wa maendeleo na makundi mengine ambayo hayajatajwa moja kwa moja na kwamba busara inahitajika katika kushughulikia sakata hilo.

Pia aliwataka wamiliki wa mashirika hayo kuepuka kuhukumu baadhi ya makundi au taasisi mpaka pale watakapokuwa na taarifa kamili au kuthibitika bila mashaka kama kundi fulani limehusika na kashfa hiyo.

Alisema ni vyema mijadala kuhusu suala hilo ungoje taarifa rasmi ya NaCoNGO, kuhusu hali halisi itakayotoa undani wa uchunguzi kwa mashirika yote yaliyohusika na tuhuma hizo, kisha taarifa yao itapelekwa katika bodi ya uratibu kupitia ofisi ya msajili wake iliyopo nchini.
 
Sitaki kuamini Mwakyembe aliamua.kuzungumza vile bila ushahidi wowote, ili kutafuta sifa za kisiasa, kwanza ule umri wake hana muda mrefu kwenye ubunge [kama bado anao hakuchakachuliwa na Magufuli].
 
Ukianza kutambulishwa Kwa 'aliwahi shika nyadhfa mbalimbali "most of times uko on your way out....
 
Wawaite wawahoji kisha washtakiwa hatutaki ushoga Tanzania

USSR
 
hii vita mwakyembe atashinda japo kwa taabu
 
[emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Shetani ana nguvu lakini Mungu ana nguvu zaidi kwa wanaomwamini na kuamini katika nguvu zake.

Shetani na wafuasi wake hawatashinda katika hili

Watashindana lakini hawatashinda

Amina.
Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…