Kakijana
JF-Expert Member
- Aug 8, 2021
- 726
- 3,345
Au amewahi ili asitajwe, na akitajwa ionekane ni siasa?Naona wanajitekenya... bora tu Lilian akae kimya... mambo ni magumu mno, they have deep roots in all systems... unless tungekuwa nchi huru
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Au amewahi ili asitajwe, na akitajwa ionekane ni siasa?Naona wanajitekenya... bora tu Lilian akae kimya... mambo ni magumu mno, they have deep roots in all systems... unless tungekuwa nchi huru
Wawaite wawahoji kisha washtakiwa hatutaki ushoga TanzaniaImeandikwa katika gezeti la NIPASHE:
BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), limeanza kuyahoji mashirika 29 yasiyo ya kiserikali (NGO), dhidi ya tuhuma iliyoibuliwa na Waziri wa zamani, Dk. Harrison Mwakyembe na baadaye kusambaa kwenye mitandao ya kijamii alizodai zinajihusisha na kampeni ya kueneza ushoga nchini.
Mwakyembe ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kwenye serikali ikiwamo Waziri wa Katiba na Sheria, alitoa taarifa hiyo kwenye mkutano ulioandaliwa na viongozi wa dini kupinga mapenzi ya jin-sia moja uliokuwa na kaulimbiu 'Tanzania bila ushoga inawezekana'.
Kwenye taarifa yake, alisema utafiti wal-ioufanya kupitia tume aliyoiunda umebaini kuna mashirika 29 yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na vitendo vya kueneza map-enzi ya jinsia moja (ushoga), jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kitanzania.
Kupitia tamko hilo lililogusa hisia za watu wengi na kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamil, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Lilian Badi alisema baada ya kuona taarifa hiyo kuna hatua kadhaa walizichukua kukabiliana na kilichoibuliwa.
“Tumeyaita na kuanza kuyahoji hayo mashirika yaliyotuhumiwa na kufanva uchunguzi wa kina na tunamuhoji Dk. Mwaky-embe ili tujue alifanyaje utafiti wake mpaka akabaini uwapo wa NGOs 29 zinazoshinikiza ushoga."
"Tulifanya kikao cha dharura cha kamati tendaji kujadili namna ya kuchunguza hali hiyo na kuweka maazimio ya utekelezaji, kufanya mawasiliano ya awali na mashirika. yote yaliyotuhumiwa kupitia utafiti huo ikiwa ni maandalizi ya kuwafanyia uchunguzi pamoja na mahojiano ya kina," alisema DK. Lilian na kuongeza
"Hatua nyingine, tumeomba kukutana na kamati ya Dk. Mwakyembe ili tupatiwe taarifa yao itusaidie kuendeleza maoni yetu na juhudi tutakazozichukua kama viongozi wa sekta na NGO."
Alisema baada ya kukamilisha hatua hizo, wataandaa taarifa ya pamoja itakayoambatana na tamko kwa umma kuweka hadharani hatua watakazozichukua.
Alitahadharisha kuwa ni vyema kutambua suala hilo ni mtambuka sio NGO pekee wanaohusika, hata serikali pia kupitia vyombo vyake, wabia wa maendeleo na makundi mengine ambayo hayajatajwa moja kwa moja na kwamba busara inahitajika katika kushughulikia sakata hilo.
Pia aliwataka wamiliki wa mashirika hayo kuepuka kuhukumu baadhi ya makundi au taasisi mpaka pale watakapokuwa na taarifa kamili au kuthibitika bila mashaka kama kundi fulani limehusika na kashfa hiyo.
Alisema ni vyema mijadala kuhusu suala hilo ungoje taarifa rasmi ya NaCoNGO, kuhusu hali halisi itakayotoa undani wa uchunguzi kwa mashirika yote yaliyohusika na tuhuma hizo, kisha taarifa yao itapelekwa katika bodi ya uratibu kupitia ofisi ya msajili wake iliyopo nchini.
hii vita mwakyembe atashinda japo kwa taabuMwanasiasa aliyewai kuwa Waziri kwenye Wizara tofauti, ikiwemo Wizara ya Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe ameitwa na Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) kueleza kwa kina kile alichoeleza mbele ya Umma kuhusu madai ya baadhi ya mashirika (NGOs) kuhusika kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini, ambapo ametumia masaa zaidi ya matatu kujieleza.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 2, 2023, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Dr. Lilian Badi, amesema Kamati Tendaji kwa kushirikiana na Kamati Ndogo ya Maadili ya Baraza hilo, imeanza kumuhoji Dr mwakyembe na kuzihoji NGO's hizo zinazotuhumiwa ili kubaini uhalisia.
"Tupo hapa Leo Kamati Tendaji ya NaCoNGO tukishirikiana na kamati ndogo ya maadili kujadili tuhuma za uwepo wa NGO's zinazoendesha masuala ya ushoga kama ilivyoelezwa na Dk. Mwakyembe. Dk. Mwakyembe atatueleza alifanyaje tafiti, amegundua nini, kwa nini aliamha kutoa taarifa. Hivyo anatoa maelezo yake yakikamilika NaCoNGO itatoa taarifa kwa umma kinaga ubaga," amesema Dk. Badi.
Aidha Dr. Lilian Badi amesema baada ya kamati hizo kumaliza kuwahoji wahusika, ikiwemo mashirika yanayotuhumiwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mashirika yatakayobainika kuhusika na vitendo hivyo, lakini pia ameweka wazi kuwa jitihada zimefanyika kuyaita mshairika yaliyotajwa kuleta taarifa ya shughuli wanazofanaya.
"Kumefanyika mawasiliano na mashirika yote yaliyoorodheshwa kwenye taarifa ya Dk. Mwakyembe, tumeomba watuletee taarifa ya shughuli wanazofanya miaka mitano iliyopita. Tumewaita kuwasikiliza na kuanza kuwahoji na kuanza uchunguzi"-M/Kiti NACoNGO, Dk. Lilian Badi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa NaCoNGO, ameitaka sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa watulivu katika kipindi ambacho Baraza hilo linafanyia kazi tuhuma zinazoibuliwa na Mwakyembe, ambapo amesisitiza kuwa NaCoNGO itaendelea kuzingatia taratibu ambazo hazikiuki sheria za Nchi sambamba na maadili.
"Kama NaCoNGO tunataka kuilinda jamii yetu na kubaki salama katika suala hili lililokinyumr na maadili. Ni vyema kuungana kuwa pamoja kuliko kunyoosheana vidole," amesema Dk. Badi.
Ikumbukwe Dk. Mwakyembe hivi karibuni mbele ya Umma alinukuliwa akitaja baadhi ya NGOs (29) akidai kuwa zihusika kueneza ushoga nchini, ambapo alidai kuwa anayo orodha na majina ya waratibu wa masuala hayo, kufuatia kauli hiyo iliibua mjadala mseto huku baadhi ya wadau wakionekana kumuunga mkono na wengine kupingana nae.
Ushoga sio mzuriTindikali kwenye ubongo sio mchezo.
[emoji122] [emoji122] [emoji122]Mwanasiasa aliyewai kuwa Waziri kwenye Wizara tofauti, ikiwemo Wizara ya Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe ameitwa na Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) kueleza kwa kina kile alichoeleza mbele ya Umma kuhusu madai ya baadhi ya mashirika (NGOs) kuhusika kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini, ambapo ametumia masaa zaidi ya matatu kujieleza.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 2, 2023, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Dr. Lilian Badi, amesema Kamati Tendaji kwa kushirikiana na Kamati Ndogo ya Maadili ya Baraza hilo, imeanza kumuhoji Dr mwakyembe na kuzihoji NGO's hizo zinazotuhumiwa ili kubaini uhalisia.
"Tupo hapa Leo Kamati Tendaji ya NaCoNGO tukishirikiana na kamati ndogo ya maadili kujadili tuhuma za uwepo wa NGO's zinazoendesha masuala ya ushoga kama ilivyoelezwa na Dk. Mwakyembe. Dk. Mwakyembe atatueleza alifanyaje tafiti, amegundua nini, kwa nini aliamha kutoa taarifa. Hivyo anatoa maelezo yake yakikamilika NaCoNGO itatoa taarifa kwa umma kinaga ubaga," amesema Dk. Badi.
Aidha Dr. Lilian Badi amesema baada ya kamati hizo kumaliza kuwahoji wahusika, ikiwemo mashirika yanayotuhumiwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mashirika yatakayobainika kuhusika na vitendo hivyo, lakini pia ameweka wazi kuwa jitihada zimefanyika kuyaita mshairika yaliyotajwa kuleta taarifa ya shughuli wanazofanaya.
"Kumefanyika mawasiliano na mashirika yote yaliyoorodheshwa kwenye taarifa ya Dk. Mwakyembe, tumeomba watuletee taarifa ya shughuli wanazofanya miaka mitano iliyopita. Tumewaita kuwasikiliza na kuanza kuwahoji na kuanza uchunguzi"-M/Kiti NACoNGO, Dk. Lilian Badi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa NaCoNGO, ameitaka sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa watulivu katika kipindi ambacho Baraza hilo linafanyia kazi tuhuma zinazoibuliwa na Mwakyembe, ambapo amesisitiza kuwa NaCoNGO itaendelea kuzingatia taratibu ambazo hazikiuki sheria za Nchi sambamba na maadili.
"Kama NaCoNGO tunataka kuilinda jamii yetu na kubaki salama katika suala hili lililokinyumr na maadili. Ni vyema kuungana kuwa pamoja kuliko kunyoosheana vidole," amesema Dk. Badi.
Ikumbukwe Dk. Mwakyembe hivi karibuni mbele ya Umma alinukuliwa akitaja baadhi ya NGOs (29) akidai kuwa zihusika kueneza ushoga nchini, ambapo alidai kuwa anayo orodha na majina ya waratibu wa masuala hayo, kufuatia kauli hiyo iliibua mjadala mseto huku baadhi ya wadau wakionekana kumuunga mkono na wengine kupingana nae.
Halafu unataka rais na spika wasome hii comment?
AminaShetani ana nguvu lakini Mungu ana nguvu zaidi kwa wanaomwamini na kuamini katika nguvu zake.
Shetani na wafuasi wake hawatashinda katika hili
Watashindana lakini hawatashinda
Amina.