Mwakyembe alitumika kumuumiza Lowassa kwenye kashfa ya Richmond

Mwakyembe alitumika kumuumiza Lowassa kwenye kashfa ya Richmond

Kwani Kyela kuna nini ?
Makuzi ya Mwakyembe kwa kiasi kikubwa yalikuwa nje ya Kyela kwa vile Marehemu baba yake alikuwa mwalimu. Hivyo alikuwa anahamahama sana. Kwa Kyela ni mtu wa kuja, ndiyo maana alikuwa anatumia nguvu nyingi kushinda uchaguzi
 
Acheni kupotosha Mwakyembe alifanya Kazi yake vzr mambo Mengine tuchukulie ni mambo ya kibidanamu Lowassa hakuwa malaika mapungufu yake hatuwezi kuyaondoa saizi yy anajua na Mungu wake

Hoja ya kamati kutomuhoji Lowasa ilishawahi kujibiwa? Unawezaje kwenda mpaka US kutafuta ukweli, halafu muhusika usimpe hizo tuhuma ajitetee?
 
Naamini pia alitumika hasa nikikumbuka;

- Alivyotoa ile ripoti yake bila kumhoji Lowassa. Mwanasheria gani unaye hukumu bila ya kutoa haki ya kusikilizwa yule unayemhukumu.

- Alivyosema wakati wa kusoma ile ripoti kuna mambo mengine anayaacha, kwani kama angeyaweka wazi nchi ingeyumba.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Mimi ninavyojua lowassa alikua anaepa kuhojiwa na nafasi ya kujitetea alipewa. Mwakyembe alifanya kazi nzuri na hilo la kuacha kutoa kila kitu hadhani naona ni kwa faida ya nchi.
Lowassa ametangulia mbele ya haki ingefaa tumuache na mungu wake maana ndiye atamhukumu kwa wema au ubaya wake. Sisi kama walimwengu hakuna ajuae kesho yake. Tumuombee lowassa mapumziko ya amani.
 
Wakati wa mjadala mkali wa kashfa ya Richmond bungeni, huku tume iliyochunguza kashfa hiyo ikibanwa kuwa haikutoa nafasi kwa watuhumiwa hasa Lowassa kujitetea, aliibuka mwenyekiti wa tume ile Mwakyembe na kusema kuwa kama watu hawaridhiki waombe kanuni zitenguliwe ili aweze kuwasilisha upya ripoti yake ili aweze kusema hata siri waliyoificha ili kuikoa serikali isiporomoke yote.

Kwa maneno hayo mimi nilliewa kuwa kumbe tume ile iliwasilisha ukweli nusu na hivyo kumtoa kafara Lowassa na mawaziri wawili ili kumwokoa rais ambaye kwa maneno ya Mwakyembe kama wangeyasema yote, ingesababisha serikali yote kuporomoka.

Kwa ufupi nilivyoelewa ni kuwa taarifa ile ilikuwa inamgusa Rais moja kwa moja na kwa maana hiyo alipaswa kuondolewa madarakani lakini akaokolewa na tume kwa kuficha siri.

Hivyo kilichofanyika ilikuwa ni kukivunja kichwa (Lowassa) kwa kosa lililofanywa na ulimi (rais). Na ndio maana katika kikao kimojawapo cha chama Lowassa alimuhoji mwenyekiti kuwa ni jambo gani ambalo yeye aililifanya ambalo yeye hakujua au kumtuma?

Ni wazi Harrison Mwakyembe alitumika na Spika Sitta kumuumiza Lowassa kwa vile Sitta na Lowassa wote walikuwa wanautaka u PM kama build up ya U-Rais wa 2015
Ndiyo akawekewa sumu na kundi la wasa ili afe yeye na homeboy wake. Ila mbi ana dhambi sana
 
Kamati ilienda hadi Marekani, lakini hapo Dodoma wakakwepa kumhoji mtu muhimu zaidi kwenye uchunguzi wao. Haikuwa haki.
 
Back
Top Bottom