Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Dk Mwakyembe, Nassari wapimana

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

Chanzo: Mwananchi

Well said mwakyembe, - Utasikilizwaje wakati aliambiwa achague mawili, kujiuzulu au kushtakiwa! Angechagua kushtakiwa basi angepata nafasi ya kumwaga mchele hadharani na kujisafisha - ilmuradi awe na ushahidi , yeye akaamua kukimbia. Ingawa hivyo hata sasa anao uhuru wa kufungua mashtaka ili ajisafishe, ningekuwa mimi nisingekubali kuchafuliwa halafu nikae kimya, hata mahakama ya dunia ningeenda.
 
Ukitaka utukanwe humu jf, ligusie swala la RICHMOMD, DOWANS na MTUKUFU LOWASA. Siasa zetu zimejaa unafiki, upinzani kwa kipindi cha miaka nane walikuwa WANAICHUKIA NYAMA YA NGURUWE ALAFU MWISHO WA SIKU, WAKAAMUA WAUNYWE MCHUZI WAKE , kwa hiyo si shangai watu waliomtukana LOWASA kwa miaka nane na kwa vinywa vyao walisema walikuwa na ushahidi kwamba jamaa ni fisadi, bila kusahau series zile za Bw Kubenea na MWANAHALISI za kila siku kumchambua Lowasa juu ya ufisadi wa RICHMOMD na DOWANS na kama haitoshi akamtuhumu LOWASA na ROSTAM wanahusika ktk kumwekea sumu Mwakyembe , leo hii eti LOWASA mtakatifu si UNAFIKI huu. Wanasiasa wametugeuza kama SIGARA KALI, sijui wametuona sisi watoto wadogo, ila si shangai kwani hata huyu wanaemwita BASHITE, siku akiwa kwao watamwita KIJANA SHUJAA MH PAUL MAKONDA, ndio siasa zetu FULL UNAFIKI.
Hahahaha! Duh jamaa umepasua jipuu,
 
Hii hoja ikirudi bungeni nyumbu wote watakimbiana hatari

Huwezi kuwa na akili timamu eti ukaanza kumtetea Lowasaa
 
Hii hoja ikirudi bungeni nyumbu wote watakimbiana hatari

Huwezi kuwa na akili timamu eti ukaanza kumtetea Lowasaa
Mahakama ya mafisadi si ipo? Kwanini Mwakyembe asiende kumshtaki Lowassa huko? Anataka mpaka wapinzani walete hoja bungeni wakati yeye ndie mwenye ushahidi wa ufisadi huo! Mi nadhani ile sumu ya Polonium inazidi kuuozesha ubongo wake, itabidi apelekwe tena nje kwa matibabu! Tangu ameteuliwa uwaziri wa habari hajaweza hata kumhoji mtuhumiwa alievamia na silaha kituo cha Clouds, na anadai hawezi kutoa ripoti ya upande mmoja kama alivyofanya katika ripoti ya Richmond!! ...hahaa, hakyaMungu huyu babu na akapimwe ubongo!
 
Kwahiyo angekuwa Hakimu, ushahidi wa upande wa mashtaka ungetosha kumfunga mshtakiwa bila kumsikiliza! Hiyo natural justice anayoidai kwa Makonda mbona hakuitoa kwa Lowasa? Hizi PhD za wanasiasa wetu kuna umuhimu wa kuzichunguza....
 
Mshtakiwa wa kesi ya Richmond ameachiwa na mahakama ya kisutu baada ya upande wa jamhuri Kushindwa kuthibitisha kosa.
 
Wamesubiri papa wa Richmond (Kikwete) ameondoka madarakani ndipo wanapeleka hoja bungeni sasa? Shame upon twit Mwakyembe & Co.
 
“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.[/QUOTE]

Sababu kama hiyo ya kutokuhoji mtuhumiwa inapatikana kwa mtu aliyekosa maadii ya kisheria na ni mtovu wa adabu za utawala bora peke yake!...tujiulize tu....Ati "...katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni..." Wao walitumwa na Bunge kwenda kuona tu??...Pesa za walipakodi walizitumia kwenda kuona tu???....nini mlishonyuma wa kuona ubadhirifu wa mali ya umma??....macho??....weledi wao kwa ufisadi uliotendeka wao kujiridhisha kuona tu unatofauti gani na kundi la wanayanganyi kuona mhalifu wakampigia makkofi????....walilisaidia nini taifa kwa kuona kwao???........Kutohoji ati kwa kuwa walijiridhisha wao kwa kuona kwao kunaisaidia nini tasnia ya sheria nna haki za binadamu???....huo ni upungufu mkubwa wa maadili ya utawala bora nchini uliolidhalilisha taifa duniani!!...halafu leo unakuja na vijembe vya watoto wa mitaani ati kunyoa kwa chupa!!?
 
“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

Hadi sasa ni miezi kadhaa imepita tangu mahakama ya mafisadi iundwe. Waziri/mbunge/aliyekuwa Waziri wa Sheria anakurupuka leo na kuropoka kuwa yupo tayari kumshughulikia MTU aliyejiuzulu kuruhusu HAKI ITENDEKE miaka 8 iliyopita.
Huyu ni Profesa msomi kweli!?
Ni nzima wa akili!?

Sent from my Vodafone 875 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom