Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Mwakyembe awatega wabunge CHADEMA, awaambia wakitaka ukweli warudishe hoja ya Richmond Bungeni

Wapinzani hawatuchezei akili acha kuwasingizia. Wanaotuchezea akili ni wale ambao tumewapa ridhaa ya kutuongoza na kuhakikisha kila mtu anatendewa kwa haki, na hawafanyi hivyo. Acha kuwapandisha hadhi wapinzani kwenye mambo ya ovyo. Put the blame where it belongs.
Mkuu mimi naeleza mawazo yangu, kwahiyo kama wewe unaona ni sawa kuwaamini basi sawa
 
Huu ndiyo upumbavue na ulofa!. Hivi huyu Kyembe zinamtosha?

Habari ya Richmond anapoiweka kwa maslahi ya kisiasa wakati taifa linaumia ni binadmau wa naman gani huyu?

Hivi habari za ufirauni unafanyika na ccm ni CHADEMA tu ndo wnaoumia?

Kwa nini wasimpeleke mahakamani na wezi wengine?

Kwa akili ya kawaida, huyu kyembe, kwa nini anang'ang'ani habari ya richmond irudishwe bungeni wakati anataarifa zote na hiyo hatua ilishapita? Kwa nini yeye kama serikali inajua ukwlei wasimpeleke mahakamani ili akahukumiwe kwa haki? Anakinmbile kusema irudi bungeni ili apate support za kipumbaveu za ndiyoooooo? Au ni kwa kuwa hata mauwongo yake akisem abungeni anakuwa na kinga?

WATANZANIA, WATU KAMA KWEYMBE HAWAFAI KWA MAENDELEO YA TAIFA.

Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Dk Mwakyembe, Nassari wapimana

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

Chanzo: Mwananchi
 
Wapinzani msiondolewe kwenye hoja za msingi na huyu jamaa, kuweni makini sana naye. Wakati ule, ni yeye aliyesema "Kamati yake ingesema kila kitu serikali ingeanguka" Someni tena Hansard, na kisha mwulizeni awaambie kwa nini alishindwa kusema kila kitu wakati huo.... Kama ni kweli aliamini EL alikuwa mhusika mkuu, na alitaka kumnyoa kwa chupa kama anavyosema leo, kwa nini alificha baadhi ya mambo????? using common sense, is a very powerful thing!!
 
Kwani kwa akili yako ni nani waliofanya figisu ambao huyo Mwakayembe anawaambia warudishe suala Bungeni?? Kwa nini hajaomba suala ya ESCROW lirudishwe pia???? au lenyewe halikuwa na figisu? Tumia akili kidogo tuu, hii siyo wala rocket science.
Na wewe pia tumia akili!

Nasari hakuhoji ishu ya escrow, alihoji suala la richmond akionesha kwamba Lowassa alionewa ndio maana mwakyembe akamjibu hivyo!

Fuatilia mambo kwa umakini.
 
Si ni huyu huyu Mwakyembe aliyesema kwamba angesoma report your Serikali ingeanguka?
Alikuwa anaficha nini,sasa anapata wapi guts now?
Kama ushahidi upon wampeleke mahakamani tujue mbivu na mbichi...lakini so kutaka kuhamisha mijadala ya binge kwa sasa wakati serikali inafail
Kwani selikali haikuanguka? Lowasa alijiuzulu u pm, ndio kusema sekikali ilianguka
 
Hata leo tunawaambia kuna mtu anaitwa Daudi Bashite anafanya kazi kwa kutumia "mavyeti" feki, but they never do anything or take any action as usual. Wanasubiri Bashite ahame chama chao ndio waanze nao kumwandama kwa vyeti feki???? You cannot be a reasonable ruling party by doing all the wrong things...Ni lazima tuwaambie ukweli hata kama unauma.
Sasa fikiri bashite aje huko chadema alafu mmpe VIP treatment! Si mtakuwa wajinga wakutupwa?
 
Na wewe pia tumia akili!

Nasari hakuhoji ishu ya escrow, alihoji suala la richmond akionesha kwamba Lowassa alionewa ndio maana mwakyembe akamjibu hivyo!

Fuatilia mambo kwa umakini.

Umeshinda Mkuu. IQ yako inaweza kuwa insignificant, kwa hiyo naweza kuwa nimevaa mkenge hapa.
 
Sasa fikiri bashite aje huko chadema alafu mmpe VIP treatment! Si mtakuwa wajinga wakutupwa?

That is the problem, you don't think outside the box. You narrow your thinking and fit yourself into Chadema's patter of doing things. Unataka nikukumbushe kwamba Chadema hawana nchi wanayoitawala katika Afrika au utajiongeza mwenyewe baadaye???
 
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.

Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!

Dk Mwakyembe, Nassari wapimana

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) na Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Dodoma. Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.

Wawili hao walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

“Huyu Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape (Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna haki hapo,” alisema.

Kauli za Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema: “Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni halafu Bunge linakuja kuamua.”

Dk Mwakyembe alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati badala yake walikuja kumshtaki bungeni.

“Huyu mtu wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.

Chanzo: Mwananchi

Huyo Mwakyembe kichwa chake kilishaharibika yupo yupo tu. Ni mgonjwa huyo. Kipindi cha Richmond yeye ndie alikuwa mwenyekiti wa kamati alishindwa nini kueleza yote. Leo anatujia na porojo za alfu lelaulela. Mwakyembe anayotamaa ya madaraka tangu kipindi cha Richmond aliaidiwa uwaziri akashindwa kutoa ripoti akachapiachapia. Leo anatujia na mafangas yake eti rudisheni Richmond. Miaka 20 inaenda alikuwa wapi kueleza. Umewadhalilisha sana wanyakyusa unapenda madaraka huwezi kusimamia ukweli unapinda kama bendera
 
mimi nafikiri ili swala sio la chadema ni la nchi mwakyembe amekua waziri wa katiba na sheria lakini hakuwahi ongelea swala la richmond sasahivi kabwana na ansad ndo anaanza kusema kama chadema wana ushahidi warudishe swalala richmond mezani swali kwanini mwakyembe mwenyewe asirudishe swala la richmond kama anaona lowasa alitakiwa kushughulikiwa na aliachwa pili kwa nini serikali isifungue kesi dhiidi ya lowasa kuhusu richmond ilo ndo swala lamsingi kwenye mahakama ya mafisadi mwakyembe alisema hakuna fisadi sasa tunakuomba mwakyembe ufungue mashtaka mahakamani ili lowasa akikutwa na ushahidi afungwe kabisa
mwakyembe bunge sio mahakama na haliwezi kumfunga lowasa kwakua ww nimwanasheria mahiri fungua kesi ya richmond hapoi utakua umelitendea haki taifa tumechoka maneno ya kisiasa tunataka action kamanikufungwa basi afungwe sio mnaleta maneno maneno hayana mana
Mkuu hao ndio wanasiasa wa siasa majitaka tulionao nchi hii!
 
Hii serikali ijiuzulu tu.

Yaani wao ndio wameshika dola na wao ndio waliofunga huo mjadala Bungeni alafu leo ndio wanaowataka wapinzani waibue swala hilo badala ya kutekeleza maazimio ya Bunge au kufungua kesi Mahakamani.

Pathetic!
Aloufungua mjadala huo ni nasari uyo mbunge kijana
 
Kha! Ndo mnamuita Dr huyo, mbona hoja zake hazina mashiko na hazistahili kuongelewa na mtu mwenye hadhi-cheti cha PHD achilia mbali nafasi aliyonayo ya uwaziri.
vigeu geu kama kinyonga, lowasa hasafishiki, wewe ulitaka alete hoja ipi ili uione inamashiko
 
FB_IMG_1492020779152.jpg
 
That is the problem, you don't think outside the box. You narrow your thinking and fit yourself into Chadema's patter of doing things. Unataka nikukumbushe kwamba Chadema hawana nchi wanayoitawala katika Afrika au utajiongeza mwenyewe baadaye???
Hivi unajua tunachojadili hapa?
 
This guy is a lair! Anaomba kesi ya Richmond kwa sababu anataka kufanya siasa. Ni chama chake mwenyewe ndicho kilichoiua hoja hiyo Bungeni wakati ule, and he should be ashamed of what he is saying. Kwa nini asililie kesi ya ESCROW ambayo ni ya juzi tu, akarudishwa Bungeni ili aonyeshe ushujaa wake??? we say it everyday... ukiwa kwenye hiki chama unakumbwa na tatizo la IQ yako kushuka kila siku....
Una maana gani mkuu kwa hili neno lair!????? Nijuavyo mimi maana ya hili neno ni mahali ambapo wanyama wa porini wanaishi sasa sijui unaunganishaje na Mwakyembe na mnyama wa porini????? Ungeamua kutumia lugha moja tu ambayo unayoielewa kamili iwe kidhungu ama kimang'ati usingejichanganya namna hii. Usiwe kama ma surrogate wa Donald Fred Trump wakibanwa wanarudisha habari za Obama. Hapa kaulizwa juu ya Richmond wewe unataka ajibu kuhusu ESCROW halafu unataka kudharau IQ za wenzako wakati wewe IQ ya kwako ni questionable.
 
Heh!huyu Nassari Leo ndo anaona mh. lowassa hakutendewa haki!? wakati kipindi mile walikuwa wakishangilia na kupiga meza lowassa akikaangwa bungeni waache unafiki
 
Back
Top Bottom