Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Namimi swala la Tanzanite naunga mkono. Mtu kama hatendewi haki na gazeti flani kwanini haendi mahakaman?Badala yake naye anakuja mitandaoni kutoa shutuma zake. Haki inatolewa mahakaman sio kwenye page za social networks.
Magazeti ambayo huwa yanafungiwa na serikali, ni nani ambaye huwa ameenda mahakamani? Wendawazimu mtupu!
 
Huyu dr amekula uporo wa nini??
1079121
 
Na yeye ajijue hana mamlaka ya kufungia chombo cha habari chochote.
Kama kimekiuka sheria akipeleke mahakamani. Ni pombe ya aina gani hawa watawala wa sasa wamenyweshwa?
 
Nadhani ana ukichaa wa aina fulani.
Kwa niaba ya wananchi wa Kyela wakiwemo wazee wetu waliotulea kwa maadili mazuri mno , naomba kuchukua nafasi hii kuomba radhi sana kwa Kauli zisizo za kibinadamu zinazoendelea kutolewa na Mbunge wetu bungeni na kwingineko , lugha hiyo chafu haiakisi Tabia zetu sisi wana Kyela , ichukuliwe kama Tabia binafsi ya Mwakyembe mwenyewe .
 
Bado natafakari niandike nini kuhusu hii kauli ya Mwakyembe, labda nipate hiyo clip, siamini kama maneno hayo yanaweza kutoka kinywani mwake.
 
huyu bwana utu uzima wake na anayo ongea unajikuta aibu unaona wewe! kwanza alisha dharaulika ile kutolewa wizara ya maana na kuletwa uku alifaa ajitafakari ila naona ndo akili inazidi dumaa tu
 
Na sisi tunawashangaa watawala wetu mpaka leo hawajatuambia wapi alipo Azory na hao wengine ilhali vyombo kiuchunguzi vipo mikononi mwao.
 
Yeah nhe,waziri wangu kumbuka maneno yako pale kawe Tanganyika packers,unataka kuniambia umeshasahau?tumo watanzania tuna kumbuka kama tembo ipo siku utajutia na kutakuwa hakuna kuombana msamaha.Umejitoa heshima na utu wako ,huna chembe ya ubinadamu(wewe uliiomba sana kipindi kile cha giza)kuwa familia na hasa watoto wa mwandishi huyu wanakuwa bila baba,maadamu wewe unarudi nyumbani na watoto wako wanakuona baba yao inatosha ,elewa watoto wa mwandishi huyu kila wanaporudi nyumbani hawamwoni baba yao(ni zaidi ya siku 500 )na hawa weshenzi wa gazeti la mwananchi wamashamsahau mwandishi wao na haukuna kabisa matangazo ya kuonyesha bado wanamkumbuka(angalia wenzao wa aljeezera bado wanawakumbuka waandishi wao waliofungwa pale misri),hili gazeti nguli kwa sasa limekuwa nalo ni domo la chama dola,but ipo siku time na history vitakuja kutuamlia.
 
Namimi swala la Tanzanite naunga mkono. Mtu kama hatendewi haki na gazeti flani kwanini haendi mahakaman?Badala yake naye anakuja mitandaoni kutoa shutuma zake. Haki inatolewa mahakaman sio kwenye page za social networks.
Yale magazei yaliyowahi kufungiwa walalamikaji ambao ni serikali walikwenda Mahakama ipi kulalamika kisha ikatoka hukumu ya kuyafungia???
 
Halafu kila jumapili unajumuika kwenye nyumba za ibada na kumwomba Mwenyezi Mungu ,na hawa so called wachungaji,mapadre wanakupa scramenti ya bwana!sometimes huwa ninafikiria sana kuhusun hizi nyumba za ibada,ni bora kusali nyumbani kwako na Mungu wako kuliko to kujumuika na waziri mwakyembe kwenye ibada,to hell na makanisa haya.
 
Dr Mwakyembe ataka watu waache kuuliza alipo Azory Gwanda.

Na:Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Source:Mtanzania Online
Hatari!
 
Huyu Jamaa sumu ilee bado ipo kichwanii...[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
 
Back
Top Bottom