Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Jamani hata wazazi wake wasiulize? wazazi wake na familia yake hawataacha kuuliza mtoto wao alivyopotea
 
Bwana Mwakyembe huyo Azron ana wazazi kama wewe huyo Azron and ndugu kama wewe nipende kukumbusha tuu hakun akitu inauma kama kumpoteza mwanao hujui yuko hai au ni mfu... Nikuambie tuu omba msamaha Azron Gwanda hakutoka kwenye mti ana familia ndugu na marafiki
 
Musiba kasema magufuli atatawala milele na milele
Unafikiri haya yanatokea kwa bahati mbaya? ndio kujizatiti kilelemi kwenyewe huko
Watu hawaelewi hayo ndiyo maandalizi ya kuzuia mawazo mbadala ya watu wengine.
 
"Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali."
Hilo jibu linaonyesha aliyepotea hana thamani yoyote mbele ya Waziri
 
Azory is dead & gone. Mwenye masikio na asikie.

Nilisikia alidakwa na kufichwa na wajeda kwenye ile operesheni ya MKIRU. Sasa sijui kama ni kweli.

Ndugu wekeni matanga tu!
 
Ningekua mhariri wa gazet la mwananchi ningesusia kuandika habar za kwako.
 
Kuna watu kumbe wangekufa ingekuwa ahueni kwa hii nchi

Ile borne marrow imejaa baada ya kufyonzwa basi anakuwa na kiburi
 
Hiviii siku hizi hawa ma-dr na ma-prof huwa wanafanya critical analysisi na reasoning ya wqnayotaka kutoa kwa jamii ya WaTz yenye vijana wakutafakari kauli zao?? Hii kauli inatofaut gani na yule mro-pokaji wa Arumeru.
 
Hivi kuna kiongozi gani wa serikali amewahi potea? Na kumbe serikali inajua maeneo yanayopoteza watu haichukui hatua,Tanzania tumepatwa.
 
Haaaaa of oll the people Mwakiembe hukupaswa kutoa hoja hafifu kiivyo maana watu wa Taifa hili walikulilia wewe kukuombea, kwa namna zote mpaka umepona. leo hii unatoa dharau za namna hiyo.

Ninachojua Mungu nimwaminie hutoa hukumu yake kwa haki na kwa wakati (ukiwa hai au mfu)
 
Kweli utu/ubinadam umepotea miongoni mwetu watanzania hasa hiki chama cha ccm!!!hivi kweli ingelikuwa ni ndugu yake Mwakyembe amepotea angesema hivyo!? Kama nchi naona kuna sehem tulikosea na sasa adhabu tunaipata vilivyo.
 
Back
Top Bottom