Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Mwakyembe amesahau alivyobabuka mwili watu walikuwa wakimuulizia pia , leo kapona anaponda wanaomuulizia Azori Gwanda ! Hii ni aibu kubwa sana !
Bora angekufa kwa ile sumu aliyopewa maana amegeuka kuwa chukizo la wanyonge. Kilangila.
 
Mbona wakitukanwa humu jukwaani huwa wanachukua hatua, au serikali huku jukwaani inaona tu ikitukanwa?
Umesema wakitutakanwa na hao unaowasema ni serikali. Je zito ni serikali?
 
Hao walio serikalini are they so special?
Mkuu serikali haiwajibiki kufuatilia swala la mtu mmoja mmoja bila ya muhusika kutoa taarifa. Ukiigusa serikali utachukukiwa hatua stahiki lkn sio serikali imuite mhariri kwanini umeandika Zito anatembea na mke wa marehem. Zito ni nani?Zito hana tofauti na wewe tindo au Misuli nk.Leo gazeti likiandika Tindo ni ana matatizo ya akili,sio jukum la serikali kulalamika. Tindo inatakiwa ukatoe taarifa kwenye mamlaka husika. Zito kaambiwa anatembea na mke wa marehem badala ya kushtaki anakimbilia tweeter au fb kutoa mikwara ya kuroga. Serikali ifanye nn?
 
Katika watu wa hovyo,ni huyu jamaa,
Kwa majibu yake,anaweza kumkana hata mama yake mzazi,
Kwamba kwa vile ubakaji upo,mama yake akibakwa watu wasihoji kwa kuwa mbona wengi wanabakwa!
 
Mbona Magufuli/Serikali ikikosolewa hamuendi mahakamani kutafta haki bali mnayafungia magazeti?
 
Karma is a bitch

Mwakyembe aangalie sana kauli zake, anafikiria familia ya Azory inajisikiaje unapokwamisha juhudi za kumpata mwenzao.
 
Eti mpaka leo watu 20 wametoa "Thanks" kwa alichokisema Mwakyembe. Hivi kasema point gani hapo. Ngoja ndugu yako apotee na uambiwe ufyate mkia, Jinsi utavyojisikia. Ma- CCM ndivyo Yalivyo.
 
Laiti angelikuwa ni ndugu yake ama mwanae sidhani kama angeliongea maneno haya,Ila maneno mtu unenayo ipo siku yatakugeukia mwenyewe
 
..mbona magazeti ambayo ni pro-wapinzani yakikosea SEREKALI inachukua hatua?

..wananchi wanataka SEREKALI ichukue hatua kwa Tanzanite kama ilivyofanya huko nyuma kwa mwanahalisi, na magazeti mengine.
Mkuki kwa nguruwe ...
 
kweli watu waache kuhoji maana ukisoma huu uzi utajua alipo kutokana na maneno ya mwakichungwa
 
Watanzania wanahofu zaidi na CCM kuliko hata hofu ya maisha na kifo!
 
Na aliacha mke mjamzito.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…