Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Mwakyembe: Marufuku kumuliza Azory Gwanda alipo. Mbona viongozi wa Serikali hamuwaulizii? Waliokashifiwa na gazeti la Tanzanite waende Mahakamani

Mbona serikali hailalamiki mahakamani ikiona imekashifiwa? Au mahakama ni kwa ajili ya wananchi tu?
 
"Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali."
Hilo jibu linaonyesha aliyepotea hana thamani yoyote mbele ya Waziri
Ina maanisha wanapajua wapi alipopotelea na watamrejeshejesha wakijiridhisha ila ikitokea bahati mbaya mauti yakamkuta huko iwe kutoka kwa watekaji au kifo cha kawaida hatarudi tena !
 
It is possible!
Azory is dead & gone. Mwenye masikio na asikie.

Nilisikia alidakwa na kufichwa na wajeda kwenye ile operesheni ya MKIRU. Sasa sijui kama ni kweli.

Ndugu wekeni matanga tu!
 
Kweli utu/ubinadam umepotea miongoni mwetu watanzania hasa hiki chama cha ccm!!!hivi kweli ingelikuwa ni ndugu yake Mwakyembe amepotea angesema hivyo!? Kama nchi naona kuna sehem tulikosea na sasa adhabu tunaipata vilivyo.
Hapana utu bado upo ila kuna kikundi kimezoea uovu mpaka wanajisifu uovu wao.
Kwani hujakwenda sehemu ukakuta watu wana wahofu wachawi na wachawi hao kujisifu hadharani uovu wao?
 
Mwanahalisi na Mawio vilifungiwa kwa sababu vilionekana vina chochea na kuchafua viongozi wa CCM. Now Tanzanite Linachafua viongozi wa upinzani ila halifungiwi wala kuchukuliwa hatua yoyote....Nchi hii bila double standard haiendi.
 
uhai wa MTU kwa sasa hauna thamani hapa nchini ndio maana tunashuhudia wengi kupotea,kuuliwa na hakuna uchunguzi wowote na leo imedhihirishwa kuwa kuhoji walipo ni UDHAIFU wa hoja
 
Dr Mwakyembe ataka watu waache kuuliza alipo Azory Gwanda.

Na:Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Source:Mtanzania Online

Viongozi gani wa serikali?
 
Huyu Dr. ashageuka poyoyo. Mungu atuhurumie, Yaani tusimuulizie mtanzania mwenzetu aliyetoweka!!! Hii maana yake Ni kuwa wamemuua siyo!!!!?
 
Dr Mwakyembe ataka watu waache kuuliza alipo Azory Gwanda.

Na:Maregesi Paul, Dodoma

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amewashangaa watu wanaofuatilia mahali alipo mwandishi wa habari Azori Gwanda.

Dk Mwakyembe ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Amesema kwamba pamoja na kwamba watu wengi wanataka kujua alipo Gwanda lazima waelewe kwamba eneo alilopotelea mwandishi huyo walipotea watu wengi wakiwamo viongozi wa Serikali.

Kutokana na hali hiyo Waziri huyo amesema watu wasiendelee kufuatilia mahali alipo mwandishi huyo kwa kuwa hilo ni suala dhaifu.

Dk Mwakyembe aliyasema hayo bungeni leo alipokuwa alihitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2018/20.

“ Pamoja na hayo Serikali itaendelea kudhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka,”amesema Dk Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Waziri huyo amewataka watu wanaokashifiwa na magazeti wakalalamike mahakamani kwa kuwa ndiko haki inakopatikana.

Source:Mtanzania Online
Ama kweli aliyeshiba leo haikumbuki njaa iliyomkuta jana!
 
Umeshasema yamekiuka taratibu na serikali ina mamlaka ya kuyafungia magazeti pale yanapokiuka taratibu. Sasa kwa Zito Gazeti limekiuka taratibu gani?Hayo malalamiko kampelekea nani?Au huko tweeter na fb ndio Serikali iliko?

Mbona wakitukanwa humu jukwaani huwa wanachukua hatua, au serikali huku jukwaani inaona tu ikitukanwa?
 
Back
Top Bottom