The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia walimu wawili kwa tuhuma za ubakaji wa wanafunzi wao katika matukio mawili tofauti, yaliyotokea wilayani Sengerema.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Machi 19, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wibroad Mutafungwa, amesema katika tukio la kwanza, Mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyampande, Edwin Temba (37), anashikiliwa kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka 16.
Tukio hilo lilitokea Februari 24, 2025, majira ya saa 5:00 usiku, nyumbani kwa mwalimu huyo wakati mwanafunzi huyo alipokwenda kutazama mchezo wa mpira wa miguu.
"Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa na desturi ya kwenda kutazama televisheni nyumbani kwa mwalimu Edwin Temba. Ndipo siku hiyo mtuhumiwa alipopata nafasi ya kumbaka. Tayari amekamatwa na baada ya upelelezi kukamilika, atafikishwa mahakamani," amesema Kamanda Mutafungwa.
Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi linawashikilia Mwalimu wa Shule ya Msingi Bukala, Daudi Ochieng (37), na mmiliki wa nyumba ya mhanga, Adon Sospeter (53), wote wakazi wa Ibisabageni, kwa tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka 10 kwa nyakati tofauti.
"Inadaiwa kuwa kuanzia Oktoba 2024 hadi Februari 2025, mmiliki wa nyumba alikokuwa akiishi mtoto huyo, Adon Sospeter, alimtendea kitendo hicho kwa kumvutia ndani ya chumba chake kwa kisingizio cha kuangalia tamthilia pamoja. Tukio hilo lilibainika Februari 2025," amesema Kamanda Mutafungwa.
Aidha, Mwalimu Daudi Ochieng naye anadaiwa kumbaka mwanafunzi huyo mnamo Februari 2025, baada ya kumuita nyumbani kwake kwa kisingizio cha kumfundisha masomo ya ziada.
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa uchunguzi unaendelea, na wahusika watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika