Mwalimu adaiwa kumpiga ngumi mwanafunzi na kumng'oa jino, eti Kisha kapata alama 29 za Hisabati

sasa sii bora huyo kapata 29 mie nakumbuka mtihani wa mathematics form one nilipata 14/100
 
Waaalimu hawa watatuulia watoto aisee

Waongezwe mishahara buana
 
Safi sana tunataka walimu kama hao....
Ningekua ndo mimi mwalimu ningeondoa meno yote hayo dadek
Yani mwanafunzi ametoa maelezo kuwa hachapwi makalioni wewe ukajifanya nunda ukampiga ngumi??
Labda asiwe mwanangu lakini kama akiwa mwanangu hiko kiganja chako kitaning'inia kikivuja damu.
 
Hawa walimu wanaleta stress zao katika kazi.
Bahati nzuri sijapata mtoto mkubwa na akafanyiwa hivyo.
Ila kama huyo angekua mtoto wangu aisee na ninavyowachukia walimu wa shule za serikali huyo mwalimu angejuta kuzaliwa.
 
Huyo mwalimu alipo fundisha wanafunzi wakapata A na kufahulu vizuri, uliwahi kuja kupost huku kumpongeza?
Kisa kutokupongezwa ndio iwe sababu ya kufumbia ukatili wa watoto!?
Hivi ni sahihi kumpiga ngumi mwanafunzi!??
 
Huyo mwalimu alipo fundisha wanafunzi wakapata A na kufahulu vizuri, uliwahi kuja kupost huku kumpongeza?
Kwa hiyo wewe tukupongeze kwa kuwa hujaiba ama kubaka? Unapofanya kitu sahihi tulia umetimiza wajibu. Siku ukibaka ama kuiba tutakuandika humu. Mwl alipofaulisha alitimiza wajibu wake hana haja ya kudai pongezi. Akikengeuka kama hivi lazima aanikwe
 
Huyo mwalimu mi ningedeal nae kimtaamtaa kama mzazi tena baada ya siku nyingi tukio kutokea. akiwa kajisahau kabisa. Nae jino ama meno mawili lazima yamtoke
Ungekosea hawa watoto wa siku hizi ukisema walimu wawache wafanye wanayotaka kama mlivyowaacha hatuna kizazi kabisa. Nchi itaharibika. Chukulia mfano watoto wa shule za kata wengi wanatoka uswahilini ambako walishashindikana maana hata wazazi wenyewe walishanyenyua mikono. Wakitoka hapo watakuja kuwa panya road. Pongezi nyingi kwa walimu wanafanya kazi iliyotukuka
 
Huenda
Wewe ndiye mwanafunzi
 
Adhabu kupewa ni sawa kabisa. Ila isiwe adhabu ya kinyama kama kumvunja meno ama kiungo chochote cha mwili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…