Aliandika Facebook Mwachieni Lissu, siasa mtaani zinoge.
MWALIMU WA ITUNGE SECONDARY KYELA,MBEYA ASHIKILIWA NA POLISI ZAIDI YA WIKI TATU BAADA YA CHAPISHO LA FACEBOOK
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Itunge iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya Anyambilile Ibrahim Mwamwile, maarufu kama Nickodem Kitalati katika mitandao ya kijamii, anaripotiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya (RCO) kwa zaidi ya wiki tatu.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kukamatwa kwa mwalimu huyo kunadaiwa kuhusishwa na chapisho aliloliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook lenye ujumbe unaosema, "Tundu Lissu aachiwe huru."
Tumefanya kila jitihada kumtafuta kiongozi wake Mr Aliko Mwaseba ambae ndiye Mkuu wa shule ya Itunge Secondary (0755 781 073) bila mafanikio.
Hata hivyo, hadi sasa Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia mwalimu huyo, wala kuthibitisha tuhuma zozote zinazomkabili.