Mwalimu ashikiliwa na Polisi kwa Wiki 3 kwa kuandika Facebook kutaka Lissu aachiwe huru

Watanzania wanapita katika Kipindi kigumu ambacho hakina mfano! Tangu wakati wa Mwalimu.
 
Mungu tunusuru na haya mashetani mauaji
Kama kweli ni Mwl wa physics, apelekewe madaftari huko huko asahihishe sababu walimu wa physics ni lulu na wachache.

Tatizo lake amejiingiza kwenye siasa mapema. Hapa ndiyo Tanganyika.
 
Aliandika Facebook Mwachieni Lissu, siasa mtaani zinoge.

MWALIMU WA ITUNGE SECONDARY KYELA,MBEYA ASHIKILIWA NA POLISI ZAIDI YA WIKI TATU BAADA YA CHAPISHO LA FACEBOOK

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Itunge iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya Anyambilile Ibrahim Mwamwile, maarufu kama Nickodem Kitalati katika mitandao ya kijamii, anaripotiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya (RCO) kwa zaidi ya wiki tatu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kukamatwa kwa mwalimu huyo kunadaiwa kuhusishwa na chapisho aliloliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook lenye ujumbe unaosema, "Tundu Lissu aachiwe huru."

Tumefanya kila jitihada kumtafuta kiongozi wake Mr Aliko Mwaseba ambae ndiye Mkuu wa shule ya Itunge Secondary (0755 781 073) bila mafanikio.

Hata hivyo, hadi sasa Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia mwalimu huyo, wala kuthibitisha tuhuma zozote zinazomkabili.

View attachment 3625935
Polis ni idara ya ccm.kama idara zingine
 
Alitoa maoni yake lakin tukumbuke Lisu yupo Mahakamani sasa kusema aachiwe huru inaweza kuonekana kama uchochezi ukizingatia aliyekamatwa ni mwanasiasa.
Hii haiwezi kuwa uchochezi ni uonezi tu,taasis mbalimbali na watu tofauti tofauti wanapaza sauti free tundu
 
Public servants’ ethics zinasema Public servants wawe na Political neutrality. Mwalimu kakosea kuleta siasa ila Hakutakiwa kukamatwa na Polisi alitakiwa awe dealt na taratibu za kiutumishi!
Kaka katika kata ya makonga wilaya ya newala kampeni meneja wa udiwani wa chama cha mapinduzi ni mwalimu shakuru na viongozi wa CUf walienda kuripoti hilo kwenye ofisi ya mkurugenzi...katibu tawala....kwa mkuu wa wilaya...nk ila hawakumfanya chechote kile mpaka uliokaitwA uchaguzi ulipoisha tu...je sheria hizo ni kwa ajili ya walimu wanaokuwa kinyume na ccm tu? Mwaka juzi napo Kuna mwalimu wa shule ya sekondar ushirika aliitwa ofisini kwa mkurugenzi na kuhojiwa kwanini yeye ni chadema? Kisa eti ana tshirt ya m4c na walishamuona kwenye mkutano wa chadema
 
Sasa kosa lake liko wapi na wakati hadi watoto wadogo wanafahamu hiyo kesi ni ya mchongo!

Mambo mengine ni ya uonevu tu. Kwa waliosoma Topic za Colonialism na Colonial Economy kule Form Three watakubaliana na mimi hili jeshi la polisi halina tofauti yoyote ile na jeshi la Wakoloni. Kiufupi ni Copy and Paste.
 
Aliandika Facebook Mwachieni Lissu, siasa mtaani zinoge.

MWALIMU WA ITUNGE SECONDARY KYELA,MBEYA ASHIKILIWA NA POLISI ZAIDI YA WIKI TATU BAADA YA CHAPISHO LA FACEBOOK

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Itunge iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya Anyambilile Ibrahim Mwamwile, maarufu kama Nickodem Kitalati katika mitandao ya kijamii, anaripotiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya (RCO) kwa zaidi ya wiki tatu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kukamatwa kwa mwalimu huyo kunadaiwa kuhusishwa na chapisho aliloliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook lenye ujumbe unaosema, "Tundu Lissu aachiwe huru."

Tumefanya kila jitihada kumtafuta kiongozi wake Mr Aliko Mwaseba ambae ndiye Mkuu wa shule ya Itunge Secondary (0755 781 073) bila mafanikio.

Hata hivyo, hadi sasa Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia mwalimu huyo, wala kuthibitisha tuhuma zozote zinazomkabili.

View attachment 3625935
Aachiliwe kwani anashikiliwa kwa uonevu na kile chama cha majambazi a.k.a ccm!
 
Vituo vya polisi vingi kuna cases za utapeli mitandaoni,nafikiri nguvu kubwa ingeelekezwa huko kutafuta hao matapeli.

Wapelelezi wanatoza hela za CDR halafu hawajishughulishi tena case inaishia hapo.
 
Sasa ndio unashikiliwa na polisi wiki tatu?

Hiyo comment ya kisiasa haina kosa lolote la kijinai. Ni uonevu tu dhidi ya vijana wa Tanzania.
Yawezekana kakamatwa kwa kosa tofauti. Nimeangalia page yake ya Facebook wala hana followers
 
Hilo kosa tofauti si waliseme? Ni hilo hilo la Lissu na hata baada ya kufuta bado wamemshikilia.

Usilete mambo ya kuhisi hapa. Wewe unajua kuliko ndugu zake na walimu wenzake wanaofuatilia?
 
Mwalimu wa Sekondari Mbeya aripotiwa kushikiliwa na Polisi kwa zaidi ya wiki tatu Mwalimu wa Shule ya Sekondari Itunge iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya, Anyambilile Ibrahim Mwamwile, anayejulikana pia kama Nickodem Kitalati katika mitandao ya kijamii, anaripotiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya (RCO) kwa zaidi ya wiki tatu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kukamatwa kwa mwalimu huyo kunadaiwa kuhusishwa na chapisho aliloliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook lenye ujumbe wa “Tundu Lissu aachiwe huru.” Licha ya Mkuu Shule ya Sekondari Itunge, Aliko Mwaseba, pamoja na Mke wa Mtuhumiwa kufika Polisi Mara kadhaa kumuwekea kufuatilia suala lake, Polisi wamegoma kumwachia.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia mwalimu huyo wala kuthibitisha tuhuma zozote zinazomkabili.

Je, unaonaje suala hili? Je, vyombo vya dola vinapaswa kutoa taarifa rasmi mapema pale mtu anaposhikiliwa kwa muda mrefu?

IMG_20260710_003534_011.jpg
 
Attachments

  • IMG_20260710_003534_011.jpg
    IMG_20260710_003534_011.jpg
    104.4 KB · Views: 12
Aliandika Facebook Mwachieni Lissu, siasa mtaani zinoge.

MWALIMU WA ITUNGE SECONDARY KYELA,MBEYA ASHIKILIWA NA POLISI ZAIDI YA WIKI TATU BAADA YA CHAPISHO LA FACEBOOK

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Itunge iliyopo wilayani Kyela, mkoani Mbeya Anyambilile Ibrahim Mwamwile, maarufu kama Nickodem Kitalati katika mitandao ya kijamii, anaripotiwa kushikiliwa na Jeshi la Polisi katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mbeya (RCO) kwa zaidi ya wiki tatu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kukamatwa kwa mwalimu huyo kunadaiwa kuhusishwa na chapisho aliloliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook lenye ujumbe unaosema, "Tundu Lissu aachiwe huru."

Tumefanya kila jitihada kumtafuta kiongozi wake Mr Aliko Mwaseba ambae ndiye Mkuu wa shule ya Itunge Secondary (0755 781 073) bila mafanikio.

Hata hivyo, hadi sasa Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi kueleza sababu za kuendelea kumshikilia mwalimu huyo, wala kuthibitisha tuhuma zozote zinazomkabili.

View attachment 3625935
Daah sometimes unajutia kuitwa Mtanzania
 
Back
Top Bottom