Mwalimu aliyewahi kunyanyaswa na Mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia

Mwalimu aliyewahi kunyanyaswa na Mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia

Tumbu

Senior Member
Joined
May 27, 2021
Posts
109
Reaction score
96
Mwalimu ambaye aliwahi kudhulumiwa fedha zake za uhamisho na akajibiwa vibaya na mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia juzi na amezikwa leo mkoani Arusha.
Mwalimu huyo alinyimwa fedha za uhamisho na alipofika kwa mkurugenzi alijibiwa vibaya na kupoteza fahamu kisha kupelekwa hospitali kwa ambulance.
Hatahivyo hakuna uhusiano wa mojakwamoja katiya ya kifo hicho na ukandamizaji wa mkurugenzi,bali siku chache kabla ya mdai huyo kukata roho alikua anasema ataenda kumuomba mkurugenzi amlipe hela zake za uhamisho.
Mwalimu huyo alilazimika kuhamishwa shule kwani alipinga wizi uliofanywa na aliyekua Mkuu wa shule(jina kapuni) na akidai anabaraka zote za mkurugenzi. Waliamua wasimlipe mwalimu huyo hela zake za uhamisho kwa kumkomoa kisa ameeleza ukweli wote TAKUKURU wa namna ambavyo hela zilikua zinaibiwa na aliyekua mkuu wa shule.

Mkuu huyo wa shule alifanya ubadhirifu wa fedha za umma bila hofu yoyote akidai hana anayemuogopa kwani anabaraka za mkurugenzi na afisa elimu wake. Hata alipoiba baadhi ya hela alisema ametumwa na mkurugenzi na afisa elimu hivyo anawapelekea mgao wao wakubwa hao. Hata baada ya kesi kupelekwa TAKUKURU mkuu huyo wa shule aliendelea kuishi kama malaika kwani alipewa cheo na kwenda kufanya kazi katika ofisi ya afisa elimu sekondari kama sehemu ya kupongezwa kwa kuwa mwizi.

Pia afisa elimu taaluma aliyeibua wizi huo alinyanyasika na kuamua kuacha kazi kwa manyanyaso aliyopitia.Baadae aliyekua mkuu wa shule mwizi akapewa nafasi ofisini hapo na kukalia kiti cha afisa elimu taaluma aliyenyanyasika na kuamua kuacha kazi kwa mazingira magumu aliyopitia. Je kama afisa ananyanyasika mpaka aamue kuacha kazi unajua ni aina gani ya majaribu aliyopitia mama yule? Mtu mishi wa kawaida ananyanyasika kiasi gani kama afisa elimu taaluma wamemnyanyasa akaikimbia ofisi na kuamua kukaa tu nyumbani?
Haya yote Ummy anayajua na hachukui hatua kama mbunge tena na waziri mwenye dhamana.
Tanga haipo salama kabisa chini ya Mayeji na afisa elimu sekondari ndugu Gwakisa.
Mh. Rais elekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi hali ni mbaya sana,rushwa ndio imetawala haki hakuna watu wako wameumizwa. Kama kwa Sabaya umeweza kwanini isiwe kwa Mayeji na Gwakisa?

Mkurugenzi Daud Mayeji nakukumbusha kwamba dhuluma haitakujenga bali itakubomoa na kukuletea balaa maishani. Kuanzia sasa huna baraka za Mungu.

Umeshirikiana na Afisa utumishi afisa elimu na washauri wako wengine kukandamiza walimu wanne katiya 17 uliowahamisha kisa hawaungi mkono wizi uliofanywa na aliyekua Mkuu wa shule ambaye ni mtu wako wa karibu sana. Ummy anajua na ameshindwa kulikabili tatizo hilo lililosababishwa na marafiki zake wa karibu sana. Mwalimu aliyeiba nirafiki sana wa Ummy Mwalimu

TAKUKURU wanazotaarifa za wizi huo na nizaidi ya mwaka na miezi takriban kumi lakini hakuna kinachoeleweka. Kila aliyetoa ushirikiano kwa TAKUKURU amenyanyaswa na mkurugenzi na afisa elimu. Maana yake nikwamba TAKUKURU wamekua sio waadilifu kwa kutoa siri za mahojiano kati yao na mashahidi.
Mamlaka husika ingilieni kati ukandamizaji wa mkurugenzi, afisa elimu na TAKUKURU Tanga Jiji.

Kwakua taifa na familia wamempoteza mtumishi na mpendwa wao,itoshe tu kusema,bwana ametoa naye ametwaa jina lake lihimidiwe, Aaaamin
 
Chanzo cha Habari tafadhali.

Japo kapicha itakuwa umetufanyia msaada mkubwa
 
Nadhani ufafanuzi sasa unaeleweka hapo. Mamlaka zote Tanga zimelala sio aliyekua RAS wala RC wote hawakua na uwezo wa kumsemea mkurugenzi wa Tanga Jiji bwana Daudi Mayeji.
Eti ndio amemuweka Ummy haogopi kitu na huko juu ana watu wake
 
Poleni.

Hii kada ya ualimu huwa wanaburuzwa sana na serikali hata chama chao cha waalimu ni kama mojawapo ya Jumuiya ya Chama Tawala.

Chama cha walimu wameshindwa kujenga solidarity kama umma wa wafanyakazi badala yake mwalimu mmoja mmoja husikika kulalamikia maslahi yao.

Inasikitisha sana.
 
Mkuu huyo wa shule alifanya ubadhirifu wa fedha za umma bila hofu yoyote akidai hana anayemuogopa kwani anabaraka za mkurugenzi na afisa elimu wake. Hata alipoiba baadhi ya hela alisema ametumwa na mkurugenzi na afisa elimu hivyo anawapelekea mgao wao wakubwa hao.
Hili nitatizo kubwa katika sehemu nyingi nchini, labda ingefaa itazamwe namna nyingine ya kudhibiti haya matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Sio jambo jema kumsemea mabaya mtumishi mwenzako ili afukuzwe kazi.
Inavyoonekana wewe ni mmoja wa watumishi wasumbufu mnao sababisha Mkurugenzi awahamishe.yaani kwa muktadha wako kila mtu ni mbaya hapo Tanga(Hii inaitwa paranoia) na muda si mrefu tuhuma zako zinaweza kuelekea nyumba za ibada na nyumbani kwa mkurugenzi.Inaonesha ukipata fursa unaweza mmchafulia taswira hata kwa watoto wake.

#Pendekezo :Samehe mara saba sabini(Biblia inassma)
 
Sio jambo jema kumsemea mabaya mtumishi mwenzako ili afukuzwe kazi.
Inavyoonekana wewe ni mmoja wa watumishi wasumbufu mnao sababisha Mkurugenzi awahamishe.yaani kwa muktadha wako kila mtu ni mbaya hapo Tanga(Hii inaitwa paranoia) na muda si mrefu tuhuma zako zinaweza kuelekea nyumba za ibada na nyumbani kwa mkurugenzi.Inaonesha ukipata fursa unaweza mmchafulia taswira hata kwa watoto wake.

#Pendekezo :Samehe mara saba sabini(Biblia inassma)
Kwa kifupi mtoa mada ana hulka zote za kuwa ni Mchawi aliyekasoro Vifaa.
 

Haki mbinguni, duniani kuna kanuni moja haijawahi badilika only the strongest one will survive and weak will perish.
Ngoja tuone kama mkurugenzi,afisa elimu na afisa utumishi kama wataishi milele
 
Poleni.

Hii kada ya ualimu huwa wanaburuzwa sana na serikali hata chama chao cha waalimu ni kama mojawapo ya Jumuiya ya Chama Tawala.

Chama cha walimu wameshindwa kujenga solidarity kama umma wa wafanyakazi badala yake mwalimu mmoja mmoja husikika kulalamikia maslahi yao.

Inasikitisha sana.
Kweli kuna shida mahali watetezi walilegeza uzi
 
Inaonekana we pia ni mwalimu
Maana hii staili ya majungu tunaijua wanayo kina nani
 
Mtu kajibiwa vibaya hadi kazimia.

Inanikumbusha usemi fulani kwamba wazaramo wakimkamata mwizi hawampigi wanamsema mpaka anakufa.
 
Katika kitu sitakuja kunyanyaswa nacho ni boss aisee, Niliwahi tukana boss mimi hatakaa aamini mbwa yule
 
Back
Top Bottom