Mwalimu ambaye aliwahi kudhulumiwa fedha zake za uhamisho na akajibiwa vibaya na mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia juzi na amezikwa leo mkoani Arusha.
Mwalimu huyo alinyimwa fedha za uhamisho na alipofika kwa mkurugenzi alijibiwa vibaya na kupoteza fahamu kisha kupelekwa hospitali kwa ambulance.
Hatahivyo hakuna uhusiano wa mojakwamoja katiya ya kifo hicho na ukandamizaji wa mkurugenzi,bali siku chache kabla ya mdai huyo kukata roho alikua anasema ataenda kumuomba mkurugenzi amlipe hela zake za uhamisho.
Mwalimu huyo alilazimika kuhamishwa shule kwani alipinga wizi uliofanywa na aliyekua Mkuu wa shule(jina kapuni) na akidai anabaraka zote za mkurugenzi. Waliamua wasimlipe mwalimu huyo hela zake za uhamisho kwa kumkomoa kisa ameeleza ukweli wote TAKUKURU wa namna ambavyo hela zilikua zinaibiwa na aliyekua mkuu wa shule.
Mkuu huyo wa shule alifanya ubadhirifu wa fedha za umma bila hofu yoyote akidai hana anayemuogopa kwani anabaraka za mkurugenzi na afisa elimu wake. Hata alipoiba baadhi ya hela alisema ametumwa na mkurugenzi na afisa elimu hivyo anawapelekea mgao wao wakubwa hao. Hata baada ya kesi kupelekwa TAKUKURU mkuu huyo wa shule aliendelea kuishi kama malaika kwani alipewa cheo na kwenda kufanya kazi katika ofisi ya afisa elimu sekondari kama sehemu ya kupongezwa kwa kuwa mwizi.
Pia afisa elimu taaluma aliyeibua wizi huo alinyanyasika na kuamua kuacha kazi kwa manyanyaso aliyopitia.Baadae aliyekua mkuu wa shule mwizi akapewa nafasi ofisini hapo na kukalia kiti cha afisa elimu taaluma aliyenyanyasika na kuamua kuacha kazi kwa mazingira magumu aliyopitia. Je kama afisa ananyanyasika mpaka aamue kuacha kazi unajua ni aina gani ya majaribu aliyopitia mama yule? Mtu mishi wa kawaida ananyanyasika kiasi gani kama afisa elimu taaluma wamemnyanyasa akaikimbia ofisi na kuamua kukaa tu nyumbani?
Haya yote Ummy anayajua na hachukui hatua kama mbunge tena na waziri mwenye dhamana.
Tanga haipo salama kabisa chini ya Mayeji na afisa elimu sekondari ndugu Gwakisa.
Mh. Rais elekeza vyombo vyako vifanye uchunguzi hali ni mbaya sana,rushwa ndio imetawala haki hakuna watu wako wameumizwa. Kama kwa Sabaya umeweza kwanini isiwe kwa Mayeji na Gwakisa?
Mkurugenzi Daud Mayeji nakukumbusha kwamba dhuluma haitakujenga bali itakubomoa na kukuletea balaa maishani. Kuanzia sasa huna baraka za Mungu.
Umeshirikiana na Afisa utumishi afisa elimu na washauri wako wengine kukandamiza walimu wanne katiya 17 uliowahamisha kisa hawaungi mkono wizi uliofanywa na aliyekua Mkuu wa shule ambaye ni mtu wako wa karibu sana. Ummy anajua na ameshindwa kulikabili tatizo hilo lililosababishwa na marafiki zake wa karibu sana. Mwalimu aliyeiba nirafiki sana wa Ummy Mwalimu
TAKUKURU wanazotaarifa za wizi huo na nizaidi ya mwaka na miezi takriban kumi lakini hakuna kinachoeleweka. Kila aliyetoa ushirikiano kwa TAKUKURU amenyanyaswa na mkurugenzi na afisa elimu. Maana yake nikwamba TAKUKURU wamekua sio waadilifu kwa kutoa siri za mahojiano kati yao na mashahidi.
Mamlaka husika ingilieni kati ukandamizaji wa mkurugenzi, afisa elimu na TAKUKURU Tanga Jiji.
Kwakua taifa na familia wamempoteza mtumishi na mpendwa wao,itoshe tu kusema,bwana ametoa naye ametwaa jina lake lihimidiwe, Aaaamin
Wakuu wa Shule hupiga pesa za Captation Fund ,
Hupiga pesa za ujenzi mbalimbali unaofanyika kwenye maeneo yao.
WANAZIPIGA JE?
Nakudokezea kidogo tu.
Kwanza ,Pesa zinazokuja mashuleni zinaingizwa kwenye akaunti ya shule.Ili pesa itoke kwenye akaunti ya shule lazima kikao cha SMT kikae.UPIGAJI UNAANZIA HAPA.
Ili uwe memba wa SMT ni lazima uwe na sifa kuu moja,UWE KAMA HAUNAZO.LAZIMA UIMBE SIFA NA UTUKUFU JUU YAKE YEYE.UKIENDA KINYUME NA HAPO.BASI WEWE SI MSHIRIKA WAKE NA HIVYO UTACHUKIWA NAYE HADI HALMASHAURI UTAONEKANA WEWE NI MKOROFI NA FURSA ZOTE ZA SEMINA,HATA HAKI ZAKO KUZIPATA MAWILI UZIPATE BAADA YA KUZISOTEA SANA AU USIZIPATE KABISA.UTAZISIKIA TU REDIONI KWA WENZAKO WAKIZIPATA.
Pili,Baada ya mkuu wa Shule kuunda SMT ya ndiyo mzee.Mikutano yao hufanyika wakati mwingine haifanyiki isipokuwa katibu wa kikao ambaye huwa mtaaluma huelekezwa na mkuu wa shule aandae taarifa ya kikao kuwa kimefanyika leo na wajumbe wameridhia kutolewa kwa kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kazi fulani.Katibu atafuata kila mtu nyumbani kwake alimwelekeza asaini Shemu yake kwa kuwa taarifa hii ni ya muhimu sana na inatakiwa kesho asubuhi ifike halmashauri.Kumbuka sifa ya wajumbe wa SMT lazima wawe watiifu kwa mkuu wa shule kwa kila kitu.Hivyo hapa watasaini bila ya kuusoma huo muhtasari.Hapa mkuu wa shule amewini anaenda siginatory wake kwenda benki kutoa pesa.
Tatu, Wakishatoa lazima mkuu wa shule apeleke madhabahuni.( Halmashauri) Mkuu wa Idara, Kama ni suala la ujenzi basi injinia wa Wilaya lazima naye achukue kilicho chake.Ile kazi iliyokuwa inatakiwa ifanyike itafanywa chini ya kiwango.Na kwa kuwa wakaguzi ni wao basi wakija kukagua ujenzi hawatumii hata dakika tatu wanaondoka na kummwagia sifa mkuu wa shule.Hadi hapo pesa ya Serikali inakuwa imeliwa.Baada ya zoezi hili kukamilika.
Wanajitokeza waalimu ladhaa hapo ofisini wanang'amua janja janja ya namna hii kuwa pesa zinaliwa.Hao ndoa huandamwa na mkuu wa shule hadi halmashauri.Kosa dogo barua za onyo kama zote
NOTE.BODI ya Shule,Ili uwe mjumbe wa bosi ya shule kwa mujibu wa Waraka uliotolewa na Wizara zimebainisha sifa kuu mbili
Kwanza ,Awe na kuwang'oa cha Elimu kuanzia kidato cha nne kuendelea
Pili,Awe mwenye kazi halali inayomuingizia kipato.
Hapa ukija napo wakuu wa shule wamechezesha wajumbe wa bosi na kuteua wale wasio na sifa ya Elimu ya kidato cha nne ili wasiweze kuhoji maswali yaliyokwenda shule ndani ya vikao Hivyo wamewachukua hata la saba tu na zaidi ya yote ni wale wenye utii mkubwa kwake Hivyo hawana cha kumhoji .Ni kama laba stempu tu.Bodi nako kuna ukakasi.Uchunguzi ukifanyika huenda wakagundua haya.
lakini je nani amfunge paka kengele? Wakaguzi watoke nje ya Wilaya .Watoke makao makuu je wataweza kufika huko kote kwa nchi nzima?
Pili, Na tabia hii inafanyika kwenye shule za vijijini ambako wanajua hata waziri kufika huko ni muhari kwa sababu ya ama umbali mrefu na miundombinu ni mibovu.
TANBIHI , SIMAANISHI KWA SHULE ZOTE ILA BAADHI TU.NA SIMAANISHI
Naweza kusahihishwa au kurekebishwa mahali nilipokuwa.